KAKUMA: Huduma za Taarifa-SIKIKA
SIKIKA
Sasisho la Mwisho: 15/11/2024
Maelezo
SIKIKA inatoa ukwaa la taarifa na mawasiliano Kakuma, Kalobeyei, na jamii inayowakaribisha wakimbizi katika eneo hilo. Vikundi vya Wasikilizaji 290 wanapokea programu ya sauti ya dakika 30-45 kila wiki ,ambayo inatengenezwa na wakimbizi na wenyeji.
SIKIKA inashughulikia mada zifuatazo na nyinginezo:
- Afya
- Usafi wa Mazingira
- Ulinzi
- Elimu
- Michezo
- Hadithi za Mafanikio
- Mazingira/Hali ya Hewa/Mabadiliko ya Tabianchi
- Makazi
- Chakula/Lishe
- Kilimo
- Tangazo la Huduma za Umma
- Haki za Wakimbizi
- Usalama na Ulinzi
Vigezo vya Kustahiki
- Kila mkimbizi,mwanachama wa jamii ya wenyeji wanaweza kujiunga na Kikundi cha Kusikiliza SIKIKA
Jinsi Huduma Zako Zinavyopatikana Ili kuwa mwanachama wa Kikundi cha Kusikiliza
- Tafadhali wasiliana na Kiongozi wa Kikundi cha Kusikiliza katika eneo lako.
Eneo
- SIKIKA ina Vikundi vya Wasikilizaji kote Kakuma, Kalobeyei, na maeneo ya jirani. Ofisi iko Kakuma, kiwanja cha 3.
Mifumo ya Maoni ya Taasisi na Masaa ya Kazi
- Baada ya kila kikao cha kusikiliza, vikundi hujadili programu na maudhui. Wanawasilisha maoni kwa chumba cha wahariri cha SIKIKA ambapo yanachambuliwa na kipindi kipya kinatengenezwa kulingana na maoni hayo.