Huduma za Taarifa
FilmAid hutoa taarifa kuhusu huduma zifuatazo:
Msaada wa Kisheria
Huduma za Jamii
- Taarifa kuhusu maisha nchini Kenya
- Taarifa kuhusu huduma za kijamii
- Taarifa kuhusu mahali na jinsi ya kupata nyaraka (taja mfano kama vile namba ya usalama wa kijamii, kibali cha kazi, leseni ya udereva, n.k.)
Huduma za Afya
- Taarifa kuhusu huduma za afya na njia za malalamiko, maoni na msaada zilizopo
- Huduma za Maji, Usafi na Mazingira (WASH)
- Taarifa kuhusu huduma za WASH
- Kukuza usafi kupitia mawasiliano ya kijamii na elimu ya afya
Shughuli za Kijamii za Burudani
- Warsha za Sanaa
- Warsha za Muziki
Elimu
- Taarifa kuhusu jinsi ya kujiandikisha shuleni
Msaada wa Kujipatia Kipato/Ajira
- Maendeleo ya ujuzi - Mafunzo ya Vyombo vya Habari (Ufundi wa Picha, Uigizaji wa Filamu) na Tiyatro kwa Mabadiliko ya Kijamii
- Taarifa kuhusu kuanzisha biashara nchini Kenya
Kurudi Nchi Asili
- Taarifa kuhusu jinsi ya kurudi kwa hiari katika nchi yako ya asili
Vigezo vya kustahiki
- Huduma hizi zinapeanwa bure bila malipo
Jinsi ya kupata huduma
- Lugha zilizopo: Kisomali, Anyuak, Oromo, Kiswahili, Nuer, Dinka
- Mlango wa eneo hili una njia ya kupandia na kushukia
- Eneo hili lina wafanyakazi wa kike
Eneo
Dadaab: Ofisi za FilmAid Kenya , Dadaab Main Office.
Ifo: Ofisi za FilmAid Kenya, uwanja wa CARE.
Dagahaley: Ofisi za FilmAid Kenya, Uwanja wa Windle International Kenya, kando ya MSF.
Hagadera; Ofisi za FilmAid Kenya , karibu na Hospitali ya IRC.
Jinsi ya kupeana maoni kwa shirika
- Simu: +254722540834
- Masaa ya kupeana maoni kutoka FilmAid- 24hrs
- Shirika litajibu kupitia simu na barua pepe
- Miadi inaweza kufanywa kupitia: +254722540834