Kupima na Chanjo ya COVID-19 - Kambi ya Wakimbizi Hagadera
International Rescue Committee (IRC)
Sasisho la Mwisho: 10/8/2023
Maelezo
Shirika la International Rescue Committee (IRC) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya imejumuisha upimaji na chanjo ya COVID-19 katika huduma za msingi za afya zinazopatikana kwa wakimbizi na jamii zinazoishi katika Kambi ya Wakimbizi ya Hagadera. Chanjo za COVID-19 ni BILA MALIPO zinapatikana kwa watu wote wanaostahiki walio tayari kupata chanjo dhidi ya COVID-19.
Huduma katika kitengo hiki
- Upimaji wa mambukizi ya ugonjwa wa COVID-19
- Chanjo ya kwanza na ya nyongeza ya kuimarisha kinga dhidi ya COVID-19.
- Vyeti vya chanjo dhidi ya korona. Unaweza kusoma maelezo haya ili kuelewa jinsi ya kupata cheti baada ya kupokea chanjo.
Wanaohitimu kupokea huduma za chanjo ya COVID-19
- Watu walio na umri wa zaidi ya miaka 18, raiawa Kenya pamoja na wakimbizi.
- Mtu anapaswa kuwa na Kitambulisho cha Kigeni/Taifa, Nambari ya Simu, Nambari ya Manifest/Resheni/hati yoyote ya utambulisho inayotambuliwa na UNHCR. IKiwa umepoteza kitambulisho chochote, soma maelezo ya kupata kipya kweny chapisho letu.
- Wanawake wajawazito zaidi ya miezi 6 na wanaonyonyesha zaidi ya wiki 6 wanaweza kupata chanjo.
- Huduma za kupima na kuzuia COVID hutolewa. Wanaopata chanjo hupata vyeti vya chanjo ya COVID-19 hapa.
Kufikia kituo cha huduma za chanjo
- Eneo hili lina wafanyakazi wa kike.
- Mahali hapa pana bafu tofauti kwa wanaume na wanawake.
- Huduma zote zilizoorodheshwa ni za bure.
- Ufafanuzi wa lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza unapatikana mara kwa mara katika eneo hili.
- Huduma zinapatikana katika lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza kwa miadi pekee.
- Huduma zinapatikana katika lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza kwa tafsiri ya simu.
- Wakalimani wa kike wanapatikana kwa lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza.
Njia za kutoa maoni au malalamishi kuhusu huduma
- Piga simu au SMS: 0701629401
- Zungumza na Wafanyakazi wa IRC katika Kituo cha Usaidizi
- Sanduku la Mapendekezo kwenye eneo la kuhudumiwa
- Barua pepe: feedback.hagadera@rescue.org
- Tembelea Ofisi za IRC za Hagadera Shirika litajibu watumiaji ambao wametoa maoni/malalamiko kupitia barua pepe, kibinafsi.
Masaa ya ufunguzi
Jumatatu:09:00 AM - 02:00 PM
Jumatano:09:00 AM - 02:00 PM
Ijumaa:09:00 AM - 02:00 PM