Riziki na Msaada wa Ajira kwa kina mama - Women Center 1
International Rescue Committee (IRC)
Sasisho la Mwisho: 10/8/2023
Maelezo
Shirika la International Rescue Committee (IRC) kupitia mipangilio ya Ulinzi na Uwezeshaji wa Wanawake (WPE) inatoa huduma mbalimbali zinazowalenga wanawake, wasichana na vijana katika kambi ya wakimbizi Hagadera.
Huduma zinazopatikana
1. Mafunzo ya ufundi: mafunzo ya ufundi stadi.
2. Warsha za kukuza ujuzi: vikundi vya mafunzo juu ya ukuzaji wa ujuzi wa biashara na ujasiriamali ; msaada wa kifedha kwa vijana na wanawake kama vile Vyama vya Akiba na Mikopo vya Vijiji
- Taarifa kuhusu kuanzisha biashara nchini Kenya; kusaidia shughuli za kujiongezea kipato; na kilimo kidogo/nchi kavu.
- Msaada kwa vikundi vya wanawake
Mahitaji ya Kustahiki au Vigezo vya Kupata Huduma
Huduma za kina mama katika Women Centre 1, hutilewa kwa kuzingatia vigezo hivi:
- Watu wazima wenye zaidi ya miaka 18
- Hakuna miadi au booking inahitajika
- Huduma hizi zinapatikana kwa walengwa wa kike.
- Huduma ni wazi na hupatikana hata kwa jamii ya LGBTQI
- Mafunzo ya GirlShine kwa wasichana wachanga ambao wanakaribia umri wa kubalehe.
Upatikanaji wa huduma katika kituo cha Women Center 3
- Lango la eneo hili lina njia panda, inaweza kupitika na Wheelchair.
- Eneo hili lina wafanyakazi wa kike.
- Mahali hapa pana bafu tofauti kwa wanaume na wanawake.
- Huduma zote zilizoorodheshwa ni za bure/ bila malipo.
- Ufafanuzi wa lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza unapatikana mara kwa mara katika eneo hili.
- Huduma zinapatikana katika lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza kwa tafsiri ya simu.
- Wakalimani wa kike wanapatikana kwa lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza.
Unakoweza kutoa malalamishi au maoni kuhusu huduma hizi
- Piga simu bila malipo kwa 0800721608 au SMS/WhatsApp - 0701629401
- Zungumza na Wafanyakazi wa IRC katika Kituo cha Usaidizi
- Sanduku la Mapendekezo
- Barua pepe: feedback.hagadera@rescue.org
- Tembelea Ofisi za IRC za Hagadera Shirika litajibu watumiaji ambao wametoa maoni/malalamiko kupitia barua pepe, kibinafsi.
Huduma hizi zinatolewa pia katika Women Center 2, iliyoko kando ya Block H-5 ndani ya kambi ya wakimbizi Hagadera pamoja na Women Center 3 iliyo karibu na Health Post E6.
Masaa ya ufunguzi
Jumatatu:08:00 AM - 05:00 PM
Jumanne:08:00 AM - 05:00 PM
Jumatano:08:00 AM - 05:00 PM
Alhamisi:08:00 AM - 05:00 PM
Ijumaa:08:00 AM - 05:00 PM