Usaidizi wa Kisheria - Refugee Consortium of Kenya

Refugee Consortium of Kenya

Sasisho la Mwisho: 7/8/2024

Maelezo

Huduma

Ushauri wa kisheria

Uwakilishi katika mahakama na vituo vya polisi

Msaada wa kuomba vibali vya kazi na leseni

Uwakilishi katika kesi za dhuluma za kijinsia na ngono

Habari kuhusu haki zako

Habari kuhusu utaratibu wa kuomba hifadhi nchini Kenya

Usaidizi wa kujaza hati za kisheria

Kusindikizwa kwa mikutano ya kisheria au kiutawala kwa maswala yanayohusiana na uhamiaji, dhuluma ya kijinsia na ngono, na Watoto

Usaidizi wa kujitayarisha kwa mahojiano ya kuomba hifadhi nchini

Uwakilishi wa kisheria katika korti na vituo vya polisi

kesi za jinai

Vyeti vya kuzaliwa, kifo na vyeti vingine vya kibinafsi

Migogoro ya familia

Huduma za kisheria kwa waathiriwa wa vita

Huduma za kisheria kwa waliotiwa mbaroni

Huduma za kisheria kwa wasio raia wan chi yoyote

Rufaa kwa wanasheria

 

Mahitaji ya Ustahiki

Huduma zote zilizoorodheshwa hutolewa bure

Huduma hutolewa kwa wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na walionyanyaswa kijinsia na ngono

 

Upatikanaji wa Huduma

 Huduma zinapatikana pia kupitia nambari za usaidizi za bure 0800720262 na 0701414978. Simu zinaweza kupigwa baada ya masaa za kazi, kwa kesi za dharura.

Kwa sababu ya ugonjwa wa COVID 19, ushauri wa kisheria unatolewa kwa mkutano uliopangwa kwa kupiga simu kwa nambari za usaidizi ama kwa kuzungumza na Msimamizi wa Ulinzi (Protection Monitor ) wa RCK. Mkutano unaweza kupangwa kibinafsi wakati wa masaa ya kazi Saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni Jumatatu hadi Ijumaa, kwa njia ya simu wakati wa masaa ya kazi Saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni Jumatatu hadi Ijumaa,, kwa njia ya barua pepe info@rckkenya.org, ama kwa kupiga simu kwa nambari +254 700865559. Huduma inapatikana bila rufaa.

Tafsiri za lugha za Oromo, Somali, Sudan Kusini, Kiingereza, na Kiswahili zinapatikana kila wakati katika ofisi yetu.

Huduma zinapatikana katika lugha zifuatazo kwa tafsiri ya simu - Kioromo, Somali, Sudan Kusini, Kiingereza na lugha za Kiswahili.

Watafsiri wa kike wanapatikana

Kiingilio cha pahali hapa kina njia panda

Pahala hapa pana wafanyikazi wa kike

Huduma zinapatikana Jumatatu hadi Ijumaa, Saa 2 asubuhi hadi Saa 5 jioni kupitia nambari za usaidizi. Jumatatu hadi Alhamisi katika ofisi ya RCK kwenye kiwanja cha LWF na ofisi ya RCK Kalobeyei. Alhamisi katika ofisi ya RCK huko Kakuma. Huduma hii hufungwa siku za sikukuu za umma. Huduma hii haipatikani wakati wa sikukuu za umma. Hata hivyo, hii inategemea jinsi kesi zilivyo. Kwa mfano, hali za dharura zinaweza kutokea.

 

Njia ya wakati wa kutoa maoni

Barua pepe, simu, mkutano mtandaoni, ama mkutano wa ana kwa ana.

Majibu yanatolewa haraka iwezekanzavyo.