Habari kuhusu njia na mahala pa kupata hati, na usaidizi wa kufanya upya hati kama vile kibali cha kufanya kazi, na leseni ya udereva; Habari kuhusu kuishi Kenya; na Habari kuhusu huduma za mitaa - Refugee Consortium of Kenya

Refugee Consortium of Kenya

Sasisho la Mwisho: 6/8/2024

Maelezo

Huduma Zinazotolewa:

  • Ushauri wa Kisheria - Mahojiano na wateja
  • Usajili wa Leseni za Biashara na Vibali, Usajili wa kampuni
  • Uwakilishi wa Kisheria Mahakamani, Kesi za kiraia, jinai na familia, uingiliaji Kati Katika Kituo cha polisi na mahakamani, kesi za ukatili wa kijinsia (SGBV), malezi ya watoto na matunzo, uangalizi, huduma za kisheria kwa waathiriwa wa ukatili, watu walioko kizuizini, watu wasio na utaifa, maombi ya uraia, uwakilishi wa ukimbizi
  • Haki, wajibu na majukumu ya watu binafsi
  • Uwakilishi wa maamuzi ya hali ya ukimbizi, mahojiano ya hifadhi, uwakilishi wa rufaa za wakimbizi
  • Usaidizi wa kuandika hati za kisheria, mikataba, hati za ushirikiano, maombi
  • Kuondoa vikwazo kwa miadi ya kisheria na utawala
  • Msaada katika kupata hati za kiraia, vyeti vya kuzaliwa, ndoa, kifo
  • Msaada Katika usajili wa vikundi vya jamii, vikundi vya kujisaidia
  • Msaada Katika kesi za upatanishi
  • Marejeo kwa mawakili wa probono

Vigezo vya Kustahiki:

Huduma hii inapatikana kwa:

  • Watu Waliohamishwa Ndani ya Nchi (IDPs)
  • Jamii Zinazowahifadhi Wakimbizi
  • Watu Wasio na Utaifa
  • Waathiriwa wa Mateso, usafirishaji haramu wa binadamu na ubaguzi
  • Watu wa LGBTQIA

Ufikiaji:

  • Unaweza kutufikia kupitia namba ya ofisi: 0701414978. Miadi inaweza kufanywa kwa kuja ofisini wakati wa saa za kazi 8:00 asubuhi - 5:00 jioni  Jumatatu hadi Alhamisi katika eneo la 3 - ofisi za RCK, karibu na eneo la UNHCR au kwa barua pepe info@rckkenya.org. 
  • Huduma zinapatikana kwa rufaa au bila rufaa.
  • Lugha Zinazopatikana: Kiarabu, Kisomali, Kidinka, Kinuer, Kiingereza, Kiswahili Kupitia simu na vituo vya kufikia huduma
  • Wakalimani wa kiume na wa kike wanapatikana
  • Wafanyakazi wa kiume na wa kike wanapatikana
  • Huduma zote ni bure bila malipo
  • Zinapatikana Jumatatu hadi Alhamisi 8:00 asubuhi - 5:00 jioni katika ofisi za RCK eneo la 3, hazipatikani siku za sikukuu

Njia za Maoni na Muda wa Kujibu:

  • Barua pepe, simu, mtandaoni, au ana kwa ana
  • Majibu yatatolewa haraka iwezekanavyo

Masaa ya ufunguzi