- Nyumbani
- Huduma
- Taarifa
- Kuhusu
Huduma
Ushauri wa Kibinafsi
Ushauri wa kikundi
Ushauri wa kifamilia
Msaada wa kihisia
Kundi la msaada
Uingiliaji kati wakati wa dharura; huduma zinazotolewa ni pamoja na ushauri wa kiakili, kiwewe na ushauri wa jumla. Nafasi salama na iliyotengwa kwa ushauri wa ana kwa ana
Kuangaliwa muda kwa muda ili kuhakikisha kuwa umepata msaada unaohitaji
wataalamu wa Wanawake wanapatikana
Mahitaji ya Ustahiki
Huduma zote zilizoorodheshwa hutolewa bure
Huduma hutolewa kwa wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na walionyanyaswa kijinsia (wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na Jamii inayotoa hifadhi kwa wakimbizi)
Upatikanaji
Huduma zinatolewa kwa lugha za Kingereza na Kiswahili. Huduma za utafsiri katika lugha za wakimbizi zinapatikana kwa usadizi wa mtafsiri. Huduma zinapatikana bila rufaa.
Tafsiri za lugha za Oromo, Somali, Sudan Kusini, Kiingereza, na Kiswahili zinapatikana kila wakati katika ofisi yetu.
Huduma zinapatikana katika lugha zifuatazo kwa tafsiri ya simu - Kioromo, Somali, Sudan Kusini, Kiingereza na lugha za Kiswahili.
Watafsiri wa kike wanapatikana
Kiingilio cha pahali hapa kina njia panda
Pahala hapa pana wafanyikazi wa kike
Huduma zote zilizoorodheshwa hutolewa bure
Huduma zinatolewa kutoka Jumatatu hadi Ijumaa: Saa 2 asubihi hadi saa 11 jioni.
Ofisi zinafungwa siku za sikukuu za umma.
Simu zinawezwa kupigwa baada ya masaa ya kazi, kwa kesi za dharura. Kwa sababu ya ugonjwa wa COVID 19, huduma za kisheria na ushauri hufanywa kupitia miadi kwa kupiga namba za RCK. Mkutano unawezwa kupangwa na mtu binafsi kuja ofisini wakati wa masaa ya kazi Saa 2 asubuhi – Saa 11 jioni Jumatatu hadi Ijumaa, kwa njia ya simu wakati wa masaa ya kazi Saa 2 asubuhi – Saa 11 jioni Jumatatu hadi Ijumaa, kwa njia ya barua pepe info@rckkenya.org, au kwa Kupiga simu kwa nambari +254 703848641.
Njia ya wakati wa kutoa maoni
Kutoa maoni kwa njia ya simu: +254733860669, +254720943164 Ofisi: Haki House, Barabara ya Ndemi, kando ya Barabara ya Kilimani, Nairobi. Simu, barua pepe, kuja ofisini binafsi.
Majibu kwa maoni yanatolewa haraka iwezekanavyo.