Serikal
i ya Kenya, katika Idara ya Huduma kwa Wakimbizi (DRS) na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani (UNHCR) huko Dadaab zitashirikiana kusajili familia zote zilizohamishwa na watu binafsi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambao taarifa yao imenakiliwa, hawana hati, na hawajasajiliwa.

Idara ya Huduma kwa Wakimbizi (DRS) jumanne Machi 7, 2023 ilirejelea tena zoezi la usajili wa wakimbizi wapya katika kambi ya Ifo, Dadaab. Awali, zoezi hilo lilikuwa limehairishwa.

Unachohitaji kujua kuhusu zoezi la usajili:

  • Lengo la zoezi hili ni kuhakikisha kwamba watu wote waliohamishwa katika kambi za wakimbizi za Dadaab ambao taarifa yao imenakiliwa, hawana hati, au hawajasajiliwa wamesajiliwa na kuandikishwa kwa njia ya kibayometriki.
  • Ratiba za usajili zitatangazwa wiki moja kabla ya zoezi kuanza na zitatumwa kupitia washirika, viongozi wa kambi na mtandao wa mawasiliano wa jamii (CWC).
  • Familia zitaratibiwa kulingana na ukubwa wa familia zao na sehemu wanamoishi. Tafadhali njoo kwa tarehe unayopaswa. Hakutakuwa na MABADILIKO YA TAREHE (KURATIBU UPYA)!
  • Watu aliyo na umri wa miaka 18 au zaidi watakaguliwa uraia wao ili kuona kama wako kwenye sajili ya Ofisi ya Kitaifa ya Usajili ya Kenya (NRB). Zoezi hili litafanyika katika Ofisi ya DRS katika kambi yako husika.
  • Watu waliomo kwenye sajili ya NRB hawatazajiliwa.
  • Zoezi la usajili litakua Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa mbili asubuhi had saa tisa alasiri.
  • Tafadhali mlete kila mtu katika familia yako kwenye ofiki ya UNHCR ili kujiandikisha.
  • Beba hati zifuatazo unapokuja kujiandikisha: Kadi ya mgao(Ration Card) Uthibitisho wa Usajili (Proof of Registration) Hati rasmi ulizonazo, kama vile paspoti, cheti cha kuzaliwa, cheti cha ndoa, cheti cha elimu, na kadhalika.

Utapata kadi mpya ya mgao, bamba chakula, na uthibitisho wa usajili, ambayo itakuwezesha kupata usaidizi unaotolewa na UNHCR na washirika.

Shughuli za kunakili taarifa za wakimbizi zitaendelea kila siku katika kambi za Ifo na Dagahaley pekee. Watu walio na mahitaji maalum watahudumiwa kwenye meza spesheli ya waathiriwa ili kujua jinsi
watakavyo weza kupata usaidizi zaidi.

Usajili ulianza katika kambi ya Ifo, na watu ambao taarifa zao zimenakiliwa watatarajiwa kuja kulingana na ratiba iliyowekwa kwenye maeneo ya umma na ikapeanwa kwa viongozi. Pia wasiliana na watu
wanaosimamia sehemu unayoishi katika kambi kuhusu tarehe zako.

Zoezi hili la usajili SI la Wakenya. Ni kwa mataifa mengine tu ambao wanatafuta hifadhi nchini Kenya.
Kifungu. 41(3)(a) ya Sheria ya Wakimbizi ya 2021 kinasema kwamba Mkenya yeyote ambaye atapatikana na hatia ya kujiandikisha kama mtafuta hifadhi au mkimbizi atatozwa faini ya Ksh 500,000 au kufungwa jela kwa miaka 3, au zote mbili.

Beba chakula na maji ya kutosha kwa ajili ya familia yako kudumu kwa siku, kwa kuwa zoezi linaweza
kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

Huduma na usaidizi wowote zinatolewa bila malipo. Mtu akikuomba pesa, malipo, au aina yoyote ya huduma, tafadhali ripoti kupitia:

  • Ofisi yoyote ya UNHCR iliyo karibu nawe
  • Piga simu kwa nambari ya simu ya UNHCR -1517, 0800720752,
    au 0715 693 578.

Tunakuhakikishia kuwa mazungumzo yako yatakua ya kisiri.

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820) ,Jumatatu hadi Ijumaa kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni