Service Image

Imesasishwa saa: 2023/03/15

Shirika la International Rescue Committee (IRC) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya imejumuisha upimaji na chanjo ya COVID-19 katika huduma za msingi za afya zinazopatikana kwa wakimbizi na jamii zinazoishi katika Kambi ya Wakimbizi ya Hagadera. Chanjo za COVID-19 ni BILA MALIPO zinapatikana kwa watu wote wanaostahiki walio tayari kupata chanjo dhidi ya COVID-19.

Huduma katika kitengo hiki

 • Upimaji wa mambukizi ya ugonjwa wa COVID-19
 • Chanjo ya kwanza na ya nyongeza ya kuimarisha kinga dhidi ya COVID-19.
 • Vyeti vya chanjo dhidi ya korona. Unaweza kusoma maelezo haya ili kuelewa jinsi ya kupata cheti baada ya kupokea chanjo. 

Wanaohitimu kupokea huduma za chanjo ya COVID-19

 • Watu walio na umri wa zaidi ya miaka 18, raiawa Kenya pamoja na wakimbizi.
 • Mtu anapaswa kuwa na Kitambulisho cha Kigeni/Taifa, Nambari ya Simu, Nambari ya Manifest/Resheni/hati yoyote ya utambulisho inayotambuliwa na UNHCR. IKiwa umepoteza kitambulisho chochote, soma maelezo ya kupata kipya kweny chapisho letu. 
 • Wanawake wajawazito zaidi ya miezi 6 na wanaonyonyesha zaidi ya wiki 6 wanaweza kupata chanjo.
 • Huduma za kupima na kuzuia COVID hutolewa. Wanaopata chanjo hupata vyeti vya chanjo ya COVID-19 hapa. 

Kufikia kituo cha huduma za chanjo

 • Eneo hili lina wafanyakazi wa kike.
 • Mahali hapa pana bafu tofauti kwa wanaume na wanawake.
 • Huduma zote zilizoorodheshwa ni za bure.
 • Ufafanuzi wa lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza unapatikana mara kwa mara katika eneo hili.
 • Huduma zinapatikana katika lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza kwa miadi pekee.
 • Huduma zinapatikana katika lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza kwa tafsiri ya simu.
 • Wakalimani wa kike wanapatikana kwa lugha za Kisomali, Kiswahili na Kiingereza.

Njia za kutoa maoni au malalamishi kuhusu huduma

 • Piga simu au SMS: 0701629401
 • Zungumza na Wafanyakazi wa IRC katika Kituo cha Usaidizi
 • Sanduku la Mapendekezo kwenye eneo la kuhudumiwa
 • Barua pepe: feedback.hagadera@rescue.org
 • Tembelea Ofisi za IRC za Hagadera Shirika litajibu watumiaji ambao wametoa maoni/malalamiko kupitia barua pepe, kibinafsi.

Kufungua Saa

Jumatatu kufungua kutoka 09:00 AM kwa 02:00 PM

Jumatano kufungua kutoka 09:00 AM kwa 02:00 PM

Ijumaa kufungua kutoka 09:00 AM kwa 02:00 PM

Maelezo ya Mawasiliano

phone: 0701629393

Anwani

Hagadera Hospital, Hagadera Refugee camp, Kenya

0.008189
40.37199349999999

Bonyeza hapa kuona anwani katika Ramani za Google.