Kujifungua mtoto huja na hisia nyingi kali, kutoka kwa msisimko na furaha hadi hofu na wasiwasi. Inaweza, hata hivyo, kusababisha jambo lisilotarajiwa: mfadhaiko.

Kwa muda wa majuma mawili hivi baada ya kujifungua, akina mama wengi hupata mabadiliko ya kihisia, ikiwa ni pamoja na kuwa na hisia za wasiwasi, kutokuwa na furaha, na uchovu. Ni kawaida kwa akina mama kuhisi uchovu au kuzidiwa wakati fulani kwa sababu wanakabiliana na mahitaji mengi mapya - na kupata usingizi kidogo.

Ikiwa kubadilika kwa hisia za mama na yeye kuwa na wasiwasi mwingi kila mara au kutokuwa na furaha ukizidi, na kudumu zaidi ya wiki mbili, kuna uwezekana kuwa mama huyo ana mfadhaiko. Wataalamu wa afya wanaiita 'Postpartum depression'.

Ikiwa unakabiliana na mfadhaiko, uwezekano wako wa kupona bila kupata matibabu uko chini.

Mfadhaiko wa baada ya kujifungua huja aje baada ya mama kujifungua?

Baada ya kujifungua, akina mama wengi hupata mabadiliko ya mhemko ambayo ni pamoja na mabadiliko ya hisia, kulia, kuhisi wasiwasi, na ugumu wa kulala. Mabadiliko ya hisia huanza siku mbili hadi tatu baada ya kujifungua na inaweza kudumu hadi wiki mbili.

Hata hivyo, kwa baadhi ya akina mama, dalili hizi zinaweza kuzaidi na kudumu kwa muda mrefu, na kusababisha mfadhaiko.

Hii inajulikana kama mfadhaiko wa baada ya kujifungua [Postpartum depression (PPD)], aina ya mfadhaiko ambao wanawake hupata baada ya kujifungua. Dalili zake ni pamoja na ugumu wa kushikamana na mtoto, kushindwa kulala, kuwa na huzuni mara nyingi, na kuwa na hasira kila mara. Sio kosa au udhaifu. Wakati mwingine ni athari tu ya kuzaa.

Akina baba pia wanaweza kukumbwa na tatizo hili. Majukumu mapya, shinikizo la kuishughulikia familia inayokua, na kukabiliana na mfadhaiko wa mzazi mwenzake ni baadhi ya mambo yanayochangia wanaume pia kupatwa na msongo wa mawazo baada ya bibi zao kuzaa. Wanaume walio na historia ya mfadhaiko na wale walio na shida za kifedha wana uwezekano mkubwa wa kukumbwa na mfadhaiko.

Kupata matibabu ya mfadhaiko baada ya kuzaa kunaweza kusaidia kudhibiti dalili na kukuza uhusiano wa karibu na mtoto.

Ni mambo gani yanaweza kuongeza hatari ya mama kupata mfadhaiko wa baada ya kujifungua?

Baadhi ya wanawake wanaweza kuwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na mfadhaiko wa baada ya kuzaa kwa sababu tofauti. Baadhi ya mambo haya ni pamoja na:

Swa_-_Postpartum_Depression_Causes.png

Picha: Baadhi ya vyanzo vya kawaida vya mfadhaiko wa baada ya kujifungua/Julisha.info

Dalili za mfadhaiko wa baada ya kujifungua (Postpartum depression) ni gani?

Dalili nyingi za mfadhaiko baada ya kujifungua ni kama zile zinazompata mwanamke aliye na mfadhaiko wakati wa ujauzito. Dalili hizi zinajadiliwa katika makala hii.

Mbali na dalili zilizojadiliwa hapo awali, baadhi ya dalili zifuatazo zinaweza kuonyesha mfadhaiko wa baada ya kujifungua:

 • Kutokuwa na hamu kwako na kwa mtoto wako (Kumpuuza mtoto) na ugumu wa kuwa na uhusiano bora na mtoto
 • Mabadiliko ya hisia kama vile kuwa na hasira kila mara, kuwa na wasiwasi mkubwa, kujilaumu, kukata tamaa, kupoteza hamu ya shughuli ulizofurahia hapo awali, mabadiliko ghafla ya hisia, kulia sana na kupatwa na hofu ghafla.
 • Kusikia aibu, kuhisi kuwa huna thamani na kujiona kuwa wewe kuwa wewe si mama mzuri.

Tazama video hii kuhusu mfadhaiko wa baada ya kujifunguaa kama ilivyojadiliwa kwenye kipindi cha ‘Health Diary’ kwenye runinga ya NTV Kenya.

Vitu vya kufanya ukiwa na mfadhaiko wa baada ya kujifungua

Ikiwa unahisi kuwa una mfadhaiko baada ya kujifungua, ni muhimu kutafuta msaada kwa sababu inaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa haitatibiwa.

Mbali na hayo, ni muhimu pia kuzingatia yafuatayo:

 • Pata mapumziko ya kutosha na jaribu kulala mtoto anapolala.
 • Zingatia kuongeza shughuli za kuboresha afya -kama vile kutembea na mtoto wako- katika utaratibu wako wa kila siku
 • Panga muda wa kuwa peke yako ili kufanya mambo unayofurahia. Unaweza kumwomba mpenzi wako au rafiki amtunze mtoto wakati huu.
 • Kula chakula chenye lishe bora ambacho kinashibisha na kunywa maji mengi ili kusaidia katika utayarishaji wa maziwa ya mama
 • Omba usaidizi kutoka kwa familia yako na marafiki
 • Epuka pombe na dawa za kulevya- pombe inaweza leta mfadhaiko na inaweza kukufanya uhisi vibaya zaidi. Inaweza pia kupitishwa kwa mtoto kupitia maziwa ya mama na kukaathiri ukuaji wake.

Je, mfadhaiko wa baada ya kujifungua unaweza kuathiri mtoto?

Mfadhaiko wa baada ya kujifungua unaweza kuathiri mtoto kwa njia zifuatazo:

 • Kuwa na matatizo ya kushikamana na mtoto wako kunaweza kusababisha kuchelewa kwa uwezo wao wa kufikiria na kuzungumza na kuwasiliana. Inaweza pia kuathiri stadi zao za kijamii (social skills).
 • Mama aliyekumbana na mfadhaiko anaweza kusahau kupeleka mtoto wake kwa uchunguzi wa kitiba na kupata chanjo za kawaida, na asitambue wakati mtoto wake ni mgonjwa. Hii inathiri afya ya mtoto
 • Watoto wanahitaji mlezi makini na anayehusika na ikiwa mama hawezi kuwahudumia, afya yao kwa ujumla, ukuaji wao unaweza kudhoofika.

Mahali pa kupata msaada ikiwa una mfadhaiko wa baada ya kujifungua

Ikiwa unashuku kuwa wewe au mtu wako wa karibu ana dalili za mfadhaiko wa baada ya kujifungua, ni muhimu kuzungumza na mfanyakazi wa afya kama vile mfanyakazi wa afya wa jamii yako, daktari au muuguzi haraka iwezekanavyo. Wahudumu hawa wa afya wamefunzwa kutambua dalili za mfadhaiko wa baada ya kuzaa na watakusaidia kupata usaidizi unaohitaji.

Kando na kupata usaidizi wa matibabu, marafiki na wanafamilia wanaweza kuwasaidia wanawake kupigana na mfadhaiko. Hii ina maana kwamba marafiki au wanafamilia pia wana jukumu la kutekeleza katika kuhakikisha kwamba mama na mtoto wako salama.

Wanafamilia wanaweza kusaidia kwa njia zifuatazo:

 • Msaidie kufanya kazi za nyumbani ili kumpatia muda zaidi wa kupumzika baada ya kujifungua
 • Msikilize na umjulishe kwamba unaelewa mahangaiko yake.
 • Msaidie akubali kile ambacho hawezi kubadilisha kwa kuzungumza naye na kutomkaripia au kumfanya aone aibu
 • Hakikisha anakula mlo kamili, analala vizuri na anapumzika vya kutosha.
 • Msaidie kuenda kununua vitu kutoka kwa maduka au sokoni
 • Anapohuzunika, mruhusu alie au azungumzie jambo linalomsumbua bila kumhukumu
 • Mpe usaidizi usio na masharti katika kuzungumza kuhusu utunzaji wa mtoto
 • Jifunze kuhusu dalili mbalimbali za mfadhaiko wa baada ya kuzaa ili uweze kumfuatilia, na iwapo atahitaji ushauri umuunganishe na mtaalamu.

Mahali pa kupata usaidizi

NAIROBI
SHIRIKA ENEONAMBARI YA SIMU
Danish Refugee Council (DRC) 

PCEA Eastleigh Church

Nambari ya simu:  0800720309 (haitozwi chochote)
Refugee Consortium of Kenya (RCK)   

Haki House, Barabara ya Ndemi.  

Kwa ushauri - Piga 0716391412 au 0703820361

National Council of Churches of Kenya (NCCK)    Jumuia Place, Barabara ya Lenana Nambari ya simu: 0704873342

Hebrew Immigrant Aid Society (HIAS) Kenya   

 1. Eastleigh 
 2. Kayole 
 3. Kawangware 
 1. Ofisi ya Eastleigh   
 • Mahali pa ofisi: Barabara ya Juja, Estate A (Nyumba namba 59)  
 • Nambari ya simu: 0773551853
 1. Ofisi ya Kayole   
 • Mahali pa ofisi: Nasra Estate. Nyuma ya Bee Center   
 • Nambari ya simu: 0700125857
 1. Ofisi ya Kawangware  
 • Nambari ya simu: 0774098627

Health and Social Economic Development (HESED) Africa   

Eastleigh Section 3 Biafra 

Nambari ya simu: 0722736637

 

KAKUMA
SHIRIKAENEONAMBARI YA SIMU
AIC Health Ministries 
 1. Kliniki ya Nalemsekon (Clinic 5) – Kakuma 2
 2. Kliniki ya Naregae  – Kalobeyei Village 2

AICHM: 0800720845 

 

Kliniki ya Nalemsekon: 0702637769 

 

Kliniki ya Naregae: 0745330015

International Rescue Committee (IRC) 

Kituo cha Afya cha Kaapoka (Main Hospital) - Kakuma 1

 

Kliniki ya Lochangamor (Clinic 4) - Kakuma 1

 

Kliniki ya Hong-Kong (Clinic 2) - Kakuma 1

 

Kliniki ya Nationokor (Clinic 6) - Kakuma 3

 

Hospitali Kuu ya Ammusait (General Hospital)- Kakuma 4

Nambari ya usaidizi:  

0792067135
Danish Refugee Council (DRC) 

Kakuma 

Nambari ya usaidizi: 0800720414

 

DADAAB
SHIRIKAENEONAMBARI YA SIMU
Kenya Red Cross Society (KRCS) Kambi ya wakimbizi ya IfoNambari ya simu: 0701494904
International Rescue Committee (IRC) Kambi ya wakimbizi ya HagaderaNambari ya simu: 0704600513 
Doctors Without Borders (MSF) Kambi ya wakimbizi ya DagahaleyNambari ya simu: 0790205727

 

Ikiwa una maswali yoyote, zungumza nasi kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info, au  kupitia WhatsApp (+254110601820) siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni.