Mwili wa mwanamke mjamzito hupitia mabadiliko mengi katika kipindi chote cha ujauzito. Mabadiliko ya kimwili na ya kihisia yanaweza kuathiri jinsi anavyohisi kujihusu, kuhusu familia yake, na kuhusu maisha yake ya kila siku. Kwa sababu hiyo, mwanamke mjamzito anaweza kupata mfadhaiko wakati wa ujauzito. Uwezekano wa kupata mfadhaiko uko juu kwa akina mama walio wajawazito kwa mara ya kwanza, wale wenye umri mdogo, akina mama wasio na waume na wanawake ambao wamepitia ukatili wa kijinsia.

Ni muhimu kutambua wakati una mfadhaiko na kupata usaidizi. Bila matibabu, mfadhaiko unaweza kusababisha matatizo wakati wa na baada ya ujauzito wako. Katika makala hii, tutaangalia sababu za mfadhaiko wakati wa ujauzito, jinsi ya kuimudu na jinsi ya kuizuia. Pia tumejumuisha maelezo kuhusu jinsi ya kupata usaidizi mtu akiwa na mfadhaiko wakati wa ujauzito.

Je, wanawake wote wajawazito wanakabiliwa na mfadhaiko?

Sio wanawake wote watakuwa na mfadhaiko wakati wa ujauzito, kila mtu ni tofauti. Hata hivyo, ni hali ya mfadhaiko kwa wanawake wajawazito ni kawaida zaidi kuliko unavyoweza kutarajia.

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), wanawake wajawazito wawili kati ya kumi huwa na mabadiliko makubwa ya hisia wakati wa ujauzito. Watu wengi wana dalili chache za msongo wa mawazo. Hali hizi zinaweza kudumu hadi mwaka baada ya kujifungua au kukomesha mimba.

Kwa nini wanawake wajawazito wanapaswa kuwa waangalifu juu ya afya yao ya akili?

Kulingana na wataalamu wa afya, dalili na matatizo ambayo huenda yakajitokeza wakati mwanamke anaposhika mimba ni kama vile kuwa na wasiwasi mkubwa, mabadiliko ya hisia, kupoteza hamu ya kula, na kujilaumu yanaweza kusababisha madhara ya muda mrefu kwa mama, watoto wachanga na familia ikiwa hayatashughulikiwa ipasavyo. Wanawake wajawazito wanaopatwa na mfadhaiko wanaweza kukosa nguvu za kujitunza, ikiwa ni pamoja na kwenda kliniki za wajawazito kabla ya kujifungua, kula vyakula bora, na kufanya mazoezi. Mfadhaiko unaweza pia kukuzuia kushikamana na mtoto wako ambaye hajazaliwa. Kuna vituo vya afya ndani na nje ya kambi za wakimbizi ambazo hutibu mfadhaiko wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.

Ni mambo gani yanayochangia mfadhaiko wakati wa ujauzito?

Kulingana na Chama cha Wanasaikolojia cha Marekani, mfadhaiko ni ugonjwa wa akili unaoathiri vibaya jinsi mtu anavyohisi, anavyofikiria na matendo yake.  Inaonyeshwa na hisia za huzuni na / au kupoteza hamu ya shughuli zilizofurahiwa hapo awali kwa zaidi ya kipindi cha wiki 2.

Wakati wa ujauzito, miili ya wanawake hupitia mabadiliko ya kibiolojia, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya homoni. Mabadiliko haya yanaweza kuathiri kemikali za ubongo na kuchangia mwanamke mjamzito kupata mfadhaiko na wasiwasi. Mwanamke aliye na historia ya kibinafsi au ya kifamilia ya mfadhaiko ana uwezekano mkubwa wa kukabiliana na mfadhaiko wakati wa ujauzito.

Zifuatazo ni baadhi ya mambo ya ndani na nje yanayoweza kuchangia msongo wa mawazo kwa wajawazito.

Mambo ya ndani

 • Kuwa na mimba isiyotarajiwa na kuhisi aibu au hatia juu yake
 • Kuwa na historia ya mfadhaiko wakati wa ujauzito katika familia au kwa mama, wakati wa ujauzito wa awali.
 • Kupoteza mimba nyingine kabla ya ujauzito wa sasa kupitia kukomesha mimba au wakati wa kujifungua.
 • Kutokuwa tayari kumpokea na kumtunza mtoto
 • Kuwa na historia ya ugonjwa sugu wakati wa ujauzito, kwa mfano, Virusi vya Ukimwi na Kifua Kikuu.
 • Mvurugano katika mahusiano yanayosababisha talaka na kutengana wakati wa ujauzito.
 • Historia ya awali ya kuwazaa watoto wafu au kuzaa watoto walio na matatizo ya kuzaliwa kama vile Down’s Syndrome, kibwiko (club foot), kakaa iliyopasuka (cleft palate) na kupooza kwa ubongo (cerebral palsy), kati ya magonjwa mengine.
 • Mimba za utotoni – vijana wa kike wenye umri mdogo na wasichana wanaopata mimba mara nyingi hukabiliana na changamoto kama vile kunyanyapaliwa, kuolewa kwa kulazimishwa, na kukataliwa na familia zao. Kwa sababu za kimataduni, baadhi yao wanaweza kutengwa. Haya yote yanaweza kuwafanya wajisikie kukosa tumaini na kujichukia.
 • Ikiwa ujauzito ulisababishwa na unyanyasaji wa kijinsia.
 • Ambapo mimba ilisababisha kupoteza kazi
 • Hofu ya kuzaa kwa sababu ya uwezekano wa kuwa na matatizo ya ujauzito na kuzaa.

Sababu za nje zinazochangia mfadhaiko na wasiwasi wakati wa ujauzito

 • Masuala ya uhusiano au ndoa, ikiwa ni pamoja na kuwa katika uhusiano wenye matatizo, kuwa na mpenzi asiyemuunga mkono, au kuwa na uhusiano mgumu na wakwe au kutengana na mpenzi.
 • Unyanyasaji wa nyumbani kama vile kudhulumiwa kikatili na mwenza ikijumuisha tabia zozote zinazotisha, kuogofya, kushtua, kuumiza, kufedhehesha, kulaumu, au kujeruhi wanawake wajawazito.
 • Kuwa na hofu ya kijamii, ambayo ni uoga wa kuchunguzwa au kuhukumiwa wakati anapofanya kazi kwa umma.
 • Matatizo ya kifedha katika familia
 • Maafa ya asili au yanayosababishwa na binadamu kama vile vita na mafuriko wakati wa ujauzito
 • Ukosefu wa usaidizi wa kijamii, au kuwa na wanafamilia wachache na marafiki ambao wanaweza kuwa pale kwa ajili yako wakati wa mahitaji
 • Kupoteza mpendwa wakati wa ujauzito

Dalili za mfadhaiko na wasiwasi wakati wa ujauzito.

Mwanamke mjamzito anaweza kupata au kuonyesha dalili zifuatazo za mfadhaiko na wasiwasi:

 • Kujitenga na watu, ikiwemo familia
 • Kukosa usingizi au kulala sana
 • Mabadiliko ya hisia kama vile kuwa na hasira kila mara, kuwa na wasiwasi, kujilaumu, kukata tamaa, kukosa kupendezwa na shughuli zilizokuwa zikifurahisha hapo awali, mabadiliko makali ya hisia na kujawa na hofu.
 • Uchovu kupita kiasi au kupoteza nguvu
 • Kuongeza uzito/kilo au kupunguza uzito
 • Wasiwasi kwamba hawatakuwa mama mzuri, na kuwa na mawazo ya kutoa mimba.
 • Kuongezeka kwa matukio ya ugonjwa na kulazwa hospitalini
 • Kujipuuza- kupuuza kazi za kimsingi za usafi kama vile kupiga mswaki, kuchana nywele na kuoga.
 • Kuvuta sigara, kunywa pombe au kutumia dawa za kulevya kama vile bangi.

SWA-_Depression_anxiety_symptoms_during_pregnancy.png

 Mchoro wa 1: Baadhi ya dalili za kawaida za mfadhaiko wakati wa ujauzito [Kutoka: Julisha.Info].

Vitu vya kufanya ikiwa una mfadhaiko wakati wa ujauzito

Pumzika vya kutosha. Usingizi ni muhimu kwa kupumzisha mwili na akili. Mbali na kupumzika, pia fanya zifuatazo:

 • Kukubali kwamba una mfadhaiko ni hatua muhimu ya kupata usaidizi.
 • Zungumza na mtu kuhusu yale unayopitia na utafute msaada. Inaweza kuwa mwanafamilia, mshirika, rafiki au mtaalamu (mshauri, mtoa huduma ya afya)
 • Ili kuepuka kuwa peke yako au kujitenga, jihusishe na watu wengine
 • Jali afya yako na lishe yako - kula milo bora na yenye kuridhisha, kunywa maji mengi na ufanye matembezi ya mazungumzo
 • Hudhuria kliniki wakati una ujauzito na baada ya kuzaa.

Je, ni msaada gani unaotolewa kwa wanawake wanaokabiliwa na mfadhaiko wakati wa ujauzito wao ?

Mbali na usaidizi wa afya ya uzazi kutoka hospitali au zahanati ya uzazi, wanafamilia au watu wanaoaminika walio karibu na mama mjamzito wanapaswa kumsaidia katika kupigana na shida ya mfadhaiko. Wana jukumu la kutekeleza katika kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.

Wanafamilia wanaweza kusaidia kwa njia zifuatazo:

 • Kufanya kazi za nyumbani ili kumpatia mama muda zaidi wa kupumzika akiwa mjamzito
 • Zungumza naye badala ya kumkosoa ili kumsaidia kukubali kile ambacho hawezi kubadilisha
 • Mkumbushe kutembelea kliniki ya akina mama wajawazito(ANC)
 • Hakikisha kuwa anakula mlo bora (balanced diet), analala vizuri, na anapumzika vya kutosha
 • Msaidie kushughulikia mambo madogo hapa na kule kama vile kuenda madukani au sokoni
 • Mruhusu alie au azungumzie jambo ambalo linamsumbua bila kumhukumu anapohisi kulia
 • Msaidie wakati wote wa ujauzito
 • Endelea kumwangalia iwapo atahitaji ushauri nasaha
 • Muunganishe na mtaalamu wa afya ya akili.

SWA-_What_to_do.png

Mchoro wa 2: Vidokezo muhimu yanayoweza kuwasaidia wanawake wajawazito  kupambana na mfadhaiko [Kutoka: Julisha.Info]

Mahali pa kupata usaidizi

[Habari za mawasiliano zilizoorodheswa hapa chini yanalenga kuwahudumia wakimbizi katika kambi tofauti za wakimbizi nchini Kenya. Tafadhali wasiliana na hospitali iliyo karibu nawe ikiwa hauko katika kambi za wakimbizi.]

Ikiwa unahisi kuwa una mfadhaiko  wakati wa ujauzito, unaweza kuwasiliana na mashirika yafuatayo, kujadili jinsi unavyohisi nao na kupewa ushauri kwa hatua zitakazofuata.

NAIROBI
SHIRIKA ENEONAMBARI YA SIMU
Danish Refugee Council (DRC) 

PCEA Eastleigh Church

Nambari ya simu:  0800720309 (haitozwi chochote)
Refugee Consortium of Kenya (RCK)   

Haki House, Barabara ya Ndemi.  

Kwa ushauri - Piga 0716391412 au 0703820361

National Council of Churches of Kenya (NCCK)    Jumuia Place, Barabara ya Lenana Nambari ya simu: 0704873342

Hebrew Immigrant Aid Society (HIAS) Kenya   

 1. Eastleigh 
 2. Kayole 
 3. Kawangware 
 1. Ofisi ya Eastleigh   
 • Mahali pa ofisi: Barabara ya Juja, Estate A (Nyumba namba 59)  
 • Nambari ya simu: 0773551853
 1. Ofisi ya Kayole   
 • Mahali pa ofisi: Nasra Estate. Nyuma ya Bee Center   
 • Nambari ya simu: 0700125857
 1. Ofisi ya Kawangware  
 • Nambari ya simu: 0774098627

Health and Social Economic Development (HESED) Africa   

Eastleigh Section 3 Biafra 

Nambari ya simu: 0722736637

 

KAKUMA
SHIRIKAENEONAMBARI YA SIMU
AIC Health Ministries 
 1. Kliniki ya Nalemsekon (Clinic 5) – Kakuma 2
 2. Kliniki ya Naregae  – Kalobeyei Village 2

AICHM: 0800720845 

 

Kliniki ya Nalemsekon: 0702637769 

 

Kliniki ya Naregae: 0745330015

International Rescue Committee (IRC) 

Kituo cha Afya cha Kaapoka (Main Hospital) - Kakuma 1

 

Kliniki ya Lochangamor (Clinic 4) - Kakuma 1

 

Kliniki ya Hong-Kong (Clinic 2) - Kakuma 1

 

Kliniki ya Nationokor (Clinic 6) - Kakuma 3

 

Hospitali Kuu ya Ammusait (General Hospital)- Kakuma 4

Nambari ya usaidizi:  

0792067135
Danish Refugee Council (DRC) 

Kakuma 

Nambari ya usaidizi: 0800720414

 

DADAAB
SHIRIKAENEONAMBARI YA SIMU
Kenya Red Cross Society (KRCS) Kambi ya wakimbizi ya IfoNambari ya simu: 0701494904
International Rescue Committee (IRC) Kambi ya wakimbizi ya HagaderaNambari ya simu: 0704600513 
Doctors Without Borders (MSF) Kambi ya wakimbizi ya DagahaleyNambari ya simu: 0790205727

 

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info, au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820) siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni.