International Rescue Committee (IRC) kupitia mradi wa ReBuild inawasaidia wakimbizi wanaoshi Nairobi kuboresha nafasi zao za kupata ajira. Mradi huu pia unawawezesha kupata mapato yanayostahili nchini Kenya. IRC inatoa wito kwa wanaovutiwa na ufadhili huu kutuma maombi yao ili kuwa miongoni mwa watakaofaidi kwa huduma mbalimbali ambazo zinalenga kuwasaidia wakimbizi na wanaotafuta hifadhi kupata vyeti kwa ujuzi wao. 

Fursa hii iko wazi kwa wakimbizi na jamii inayotoa hifadhi ya wakimbizi wenye ujuzi wa kiufundi lakini wamefungiwa nafasi za ajira kwa kukosa vyeti vinavyofaa. 

ReBuild pia inalenga kusaidia wakimbizi au watafuta hifadhi wenye vyeti vya kufuzu kutoka nchini mwao lakini havijatambuliwa nchini Kenya. Watakaofanikiwa kupata nafasi hii watasaidiwa kupata kibali cha mashirika ya serikali ili kutumia vyeti hivyo nchini Kenya. 

ReBuild ni mradi wa aina gani? 

ReBuild ni mradi unaosaidia wakimbizi wa mijini na jamii zinazowakaribisha jijini Nairobi ili kufikia uwezo wa kujitegemea kiuchumi kupitia masuluhisho kwa kuimarisha ubinifu na riziki. 

Mechanics.jpg

ReBuild inatazamia kutambua watu wanaotimiza vigezo tofauti kwa kuwapa fursa yakutuma maombi ya kujiandikisha katika mpango wa usaidizi wa kupata riziki. 

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya washirika (Non-governmental Organizations), Mashirika yanayoongozwa na wakimbizi (Refugee Led Organizations), na Mashirika ya kijamii (Community Based Organizations) pia yanakaribishwa kupendekeza majina ya watu wanaostahiki usaidizi huukulingana na vigezo vilivyo hapa chini. 

 1. Uthibitisho wa Ujuzi 

Huduma hii hutolewa kwa watu ambao wana ujuzi fulani kama vile useremala, uchomeleaji, ushonaji, nywele na urembo, sanaa na ufundi, ufundi magari na ujuzi wowote unaoweza kuwasaidia kujikimu kimaisha lakini hawajapata cheti cha ujuzi huo. Udhibitisho hutolewa kupitia mashirika tofauti ya uthibitishaji. 

Vigezo vya uthibitisho wa ujuzi: 

 • Awe mtafuta hifadhi au mkimbizi.
 • Lazima awe na vitambulisho halali; Watafuta  hifadhi wanapaswa kusajiliwa na Idara ya Huduma za Wakimbizi- DRS pamoja na UNHCR kama wakazi wa Nairobi na si wakaaji wa kambi.
 • Awe na umri wa angalau miaka 18.
 • Uwezo wa kuzungumza Kiingereza au Kiswahili katika kiwango cha mazungumzo.
 • Uishi Nairobi na maeneo ya Kajiado ikijumuisha Eastleigh, Ngara, Huruma, Mathare, CBD, Kariobangi, Njiru Umoja, Kayole, Donholm, Jogoo Road, Embakasi, Kasarani, Ruai, Utawala, Mwiki, Githurai, Ruiru, Kawangware, Kabiria, Kibra, Kikuyu, Kangemi, Kabete, Rongai, Kitengela, Kiserian, Ngong, Matasia, nk.
 • Awe na ujuzi unaoweza kuthibitishwa kama vile ushonaji, ususi na urembo, mekanika, kuchomelea vyuma, ufundi, upishi .
 • Asiwe amewahi kupokea usaidizi wa IRC kwa huduma yoyote ya kujikimu kimaisha hapo mbeleni.
 1. Uthibitisho wa uhalisi wa vyeti 

Huduma hii inatolewa kwa wakimbizi walio na vyeti vya chuo kikuu/vyuo/taasisi ya ufundi kutoka nchi zao na bado hawajatambuliwa na serikali ya Kenya. Baada ya kuidhinishwa na mashirika ya serikali, vyeti hivi vitatambulika katika wanapotafuta ajira nchini Kenya. Hili litasaidia walio na vyeti kuongeza nafasi zao za kuajiriwa nchini Kenya. 

Vigezo vya Uidhinishaji wa vyeti 

 • Awe mtafuta hifadhi au mkimbizi.
 • Lazima awe na hati halali. Waombaji hifadhi wanapaswa kusajiliwa na DRS na UNHCR kama wakazi wa mijini na si wakaaji wa kambi.
 • Awe na umri wa angalau miaka 18
 • Uwezo wa kuzungumza Kiingereza au Kiswahili katika kiwango cha mazungumzo
 • Mkazi wa Nairobi na maeneo ya Kajiado ikijumuisha Eastleigh, Ngara, Huruma, Mathare, CBD, Kariobangi, Njiru Umoja, Kayole, Donholm, Jogoo Road, Embakasi, Kasarani, Ruai, Utawala, Mwiki, Githurai, Ruiru, Kawangware, Kabiria, Kibra, Kikuyu, Kangemi, Kabete, Rongai, Kitengela, Kiserian, Ngong, Matasia.
 • Idhinishwe na chuo kikuu/chuo/taasisi ya ufundi kutoka nchi zao za asili
 • Asiwe amewahi kupokea usaidizi wa IRC kwa huduma yoyote ya kujikimu kimaisha hapo mbeleni.

Tailoring.jpg

Vidokezo Muhimu 

 • Huduma zote ni BILA MALIPO. Hakuna malipo kwa ajili ya maombi au kujiandikisha katika mpango.
 • Waliovutiwa na nafasi hii watahitaji kuwasilisha nakala za kitambulisho au hati za usajili kwa IRC

Jinsi ya Kutuma Maombi 

Watu ambao wanakidhi vigezo vya kujiandikisha wanaalikwa kuwasilisha stakabadhi zao kwa ofisi za IRC katika maeneo yafuatayo mjini Nairobi: 

 • Jengo la Kenya Community Development Foundation (KCDF), Barabara ya Chai, eneo la Pangani
 • Times Arcade, kando ya Barabara ya Magadi huko Rongai
 • Kivuli Centre, Kabiria

Mashirika ya aina ya NGOs, RLOs na CBOs wanaalikwa kuwasilisha majina pamoja na pendekezo la kushirikisha wateja wao  kutumia fomu ya rufaa kando na kuwasilishwa kupitia barua pepe. 

Maswali na marejeleo yote yanaweza kufanywa kupitia barua pepe kwa: re-buildkenya.clientregistration@rescue.org na kunakiliwa kwa: moses.onyancha@rescue.org, au piga simu kwa: 0799 342 337/0799 342 338. 

 

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820) ,Jumatatu hadi Jumamosi kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni