Julisha.Info imepanua chaneli zake za kushiriki jumbe muhimu mtandaoni ikiwa ni pamoja na mawasiliano kwenye WhatsApp!

Unawezaje kuwasiliana na Julisha.Info kupitia WhatsApp?

  1. Hifadhi nambari ya WhatsApp ya Julisha.Info (+254110601820) kwenye orodha yako ya anwani za rununu. Ukishahifadhi nambari hii, utaweza:
  • Kututumia ujumbe wa maandishi au kwa kurekodi sauti yako.
  • Kutuma picha, faili na hata video kwetu.

Hata hivyo, hatutaweza kupokea simu yako ya WhatsApp au kukupigia tena. Mawasiliano yote yatafanywa kwa njia ya meseji kwenye WhatsApp.

  • Ikiwa huna WhatsApp; bonyeza hapa ili kuipata kwenye simu yako ya Android. Ikiwa unatumia iPhone, unaweza kubonyeza hapa kupaata WhatsApp kwa iOS.

Saa za kutuma ujumbe kwenye WhatsApp kwa Julisha

Tunapatikana kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Ikiwa hutapata jibu kutoka kwetu wikendi, wasiliana nasi Jumatatu kwa usaidizi.

mceclip0.png

Mradi wa Julisha.Info,huduma na manufaa yake

Julisha.Info ni mradi wa Signpost ambao International Rescue Committee (IRC) inatekeleza nchini Kenya ili kuwawezesha wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na jumuiya inayowapokea kufanya maamuzi muhimu kuhusu masuala ambayo ni muhimu zaidi kwao. Ni mfumo wa kidijitali wa njia mbili wa mawasiliano ambao hutoa taarifa muhimu kuhusu COVID-19, ufikiaji na upatikanaji wa huduma (kama vile afya, sheria, chakula, nyaraka, nafasi za kazi), sera za serikali na mahitaji mengine ya maelezo ya mtumiaji jijini Nairobi. , kambi ya wakimbizi ya Kakuma na kambi ya wakimbizi ya Dadaab.

Julisha.Info ina tovuti ambayo ina makala ya jumbe muhimu, ukurasa wa Facebook ulio na machapisho ya habari na ramani ya huduma ya kuwaelekeza watumiaji kwa watoa huduma. Maudhui haya yanapatikana katika lugha za Kiingereza, Kisomali, Kiarabu na Kiswahili. Unaweza kusoma zaidi kuhusu Julisha.Info katika chapisho hili.

Unaweza kuzungumza nasi na kupata taarifa kuhusu maeneo kama vile:

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820) ,Jumatatu hadi Jumamosi kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni