Akaunti ya benki ndicho chombo msingi utakachohitaji ili kutuma na kupokea pesa kwa njia salama. Kuwa na akaunti ya benki pia hukusaidia kuweka rekodi wazi ya kile unachopokea au kupata kama mapato. Kuna taasisi nyingi za kifedha nchini Kenya zinazokuruhusu kufungua akaunti ya benki, kupokea, kuweka na kutoa pesa na wakati fulani, unaweza kulipwa riba kwa pesa unazohifadhi.

SWA_Opening_bank_account.png

Katika makala haya, tutakuongoza kwenye mchakato na mahitaji ya kufungua akaunti katika benki za kawaida nchini Kenya. Mnamo mwaka wa 2017, Benki Kuu ya Kenya (CBK) iliagiza benki zote za biashara nchini kudai vyeti vya KRA kwa ajili ya kufungua akaunti yoyote mpya ya benki. Hata hivyo, angizo hilo halitumiki kwa wakimbizi wanaoishi katika kambi za Kakuma na Dadaab, ambapo wanaweza kufungua akaunti za benki katika Equity na Kenya Commercial Bank bila vyeti vya KRA.

 • Kufungua akaunti ya benki katika Kambi za Wakimbizi za Dadaab na Kakuma

Iwapo unaishi Kakuma au Dadaab, utaulizwa uthibitisho wa usajili kama mkimbizi (Manifest). Wasilisha hati hii katika benki ya Equity au KCB iliyo karibu nawe ili ufungue akaunti. Maafisa wa benki watakuchukua picha ya saizi ya pasipoti ili waweke kwa rekodi zao. Huduma hii inatolewa na benki bila malipo.Katika kambi ya Dadaab, ni benki ya Equity pekee ambayo ina tawi linalofanya kazi kuanzia Januari 2022 huku KCB ikipatikana katika mji wa Garissa ulioko kwenye Corner House, Lt Tumbo Road, karibu na mzunguko mkuu (Roundabout).

Hata hivyo, ikiwa unafungua akaunti ya benki nje ya Kakuma au Dadaab cheti cha KRA kinahitajika.Julisha.Info ina mwongozo wa jinsi ya kutuma maombi na kupata Cheti cha PIN cha KRA kama mkimbizi na kinapatikana hapa.

Kufungua Benki ya Equity, Akaunti ya Benki ya Absa - mahitaji kwa wakimbizi walioko Nairobi

Mahitaji ya kufungua akaunti ya benki na Benki ya Equity na Absa yanafanana. Unaweza kufungua akaunti ya benki katika Benki ya Equity au tawi la Absa lililo karibu nawe. Yafuatayo ni mahitaji ya kufungua akaunti ya benki. Tafadhali kumbuka kuwa lazima uwepo kwenye tawi la benki husika ili kukamilisha mchakato huu.

 • Kitambulisho cha Mkimbizi - nakala halisi itahitajika. Pia unaweza beba nakala nyingine ili ukuwe na kazi rahisi.
 • Barua za utambulizi kutoka UNHCR na RAS au Hati ya Kusafiri kwa Wakimbizi/Hati ya Kawaida ya Kusafiri (CTD).
 • Nakala ya cheti cha PIN cha Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA).
 • Picha ya pasipoti - hii itachukuliwa kwenye benki na afisa anayekusaidia kufungua akaunti yako.

Maafisa wa benki katika tawi unalotembelea watakuongoza kufungua akaunti yako ya benki. Ukiwa kwenye benki, unaweza kuomba huduma za benki ya simu ili kukuwezesha kufanya shughuli za benki kutoka kwa simu yako.

Baada ya kukamilisha mchakato huu, utapewa kadi yenye maelezo ya akaunti ya benki kama vile nambari ya akaunti yako ya benki, jina na tawi lako.Unaweza kuwasiliana na Benki ya Absa kupitia mitandao ya kijamii kwenye Twitter au Facebook. Vinginevyo, unaweza kupiga nambari +254732130120 au wasiliana nao kwenye WhatsApp +254710130000. Maswali kwa benki ya Equity yanaweza kutumwa kwa benki kwa kutumia Facebook, Twitter au kwa njia nyingine mtu anaweza kupiga 0763 063000. Unaweza pia kutuma barua pepe kwa benki kupitia info@equitybank.

 

Kufungua akaunti na benki ya Kenya Commercial Bank (KCB) - mahitaji kwa wakimbizi walio Nairobi

Benki ya KCB ina mahitaji ya ziada ya kibali cha kufanya kazi nchini Kenya wakati wa kufungua akaunti ya benki kama mkimbizi. Mahitaji kuu ni:Kitambulisho chako cha MkimbiziCheti chako cha PIN cha Mamlaka ya Mapato ya Kenya.Kibali cha kufanya kazi: Daraja la M- Kibali hiki kinatolewa kwa mtu ambaye amepewa hadhi ya mkimbizi nchini Kenya. Unaweza kubonyeza hapa ili kujifunza jinsi ya kuomba kibali hiki.

Maafisa wa benki watachukua picha yako ya pasipoti. Hii inafanywa bila malipo katika benki.Watu ambao wamepata Vyeti vyao vya PIN ya KRA na wako Dadaab au Kakuma bado wanaruhusiwa kutumia KRA Pin wanapofungua akaunti za benki.

Je, nitapataje kadi ya ATM?

ATM ni mashine inayojiendesha na mara nyingi hutumiwa kutoa pesa. Kadi za ATM hutumiwa kuwezesha hili kwa kuwa zinabeba maelezo ya benki ya mwenye akaunti ya benki. Baadhi ya benki huwaruhusu wateja wao kuweka akiba ya fedha kwa kutumia kadi zao za ATM.

SWA_opening.png

Kadi ya ATM itakuwezesha kutoa pesa kwa ajenti wa benki iliyo karibu nawe au mashine za ATM bila kulazimika kutembelea benki.Ili kupata kadi ya ATM, utahitaji kuijulisha benki yako siku utakapofungua akaunti yako ya benki. Vinginevyo, unaweza kutembelea tawi lililo karibu nawe na uombe kupewa kadi ya ATM. Benki nyingi hutoza shilingi 600 kutengeneza kadi za ATM.

Utapewa PIN maalum ambayo utaitumia kulinda na kuwa na udhibiti kamili wa matumizi ya kadi yako ya ATM. Usiambie mtu yeyote nambari yako ya PIN.Inachukua saa chache au muda usiozidi wiki moja ili kadi ya ATM kuwa tayari kulingana na benki utakayochagua kujisajili nayo.

Benki mbalimbali pia zina maajenti katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya ununuzi na katika maeneo ya makazi ya Nairobi, Kakuma na Dadaab. Maajenti hawa hutoa huduma kama vile:

 • Kuweka pesa au kutoa pesa kwenye akaunti
 • Kulipa karo ya shule
 • Malipo ya bili kama vile kodi, umeme na maji
 • Kujua salio la akaunti yako ya benki
 • Kufungua akaunti ya benki
 • Kulipa NHIF, NSSF na KRA
 • Ukusanyaji wa kadi za ATM

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info, Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 08:00 asubuhi hadi 5:00 asubuhi.