Jinsi ya kulinda watoto wanaonyonya dhidi ya janga la COVID-19

Vitu vingine rahisi kama vile kunyonyesha vinaweza kuokoa watoto milioni kwa mwaka. Hii ndio sababu siku saba za Agosti kila mwaka wiki ya kunyonyesha imewekwa alama ulimwenguni kote ili kujenga ufahamu kuhusu umuhimu wa unyonyeshaji kwa watoto wachanga.

Maziwa ya mama ni chanzo bora cha lishe kwa watoto na inawalinda dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika. Kunyonyesha kunatosheleza mahitaji yote ya kimsingi ya watoto wachanga. Watoto wachanga hupata joto wakiwa mikononi mwa mama wakati wananyonyeshwa. Maziwa ya mama ni chakula chao na chanzo cha usalama wakati wanajua uwepo wa mama.

Zaidi ya hapo awali, unyonyeshaji unapaswa kuhimizwa wakati wa janga hili la COVID-19 kwani ndio njia bora ya kuzuia watoto wachanga wakati wa janga hili.

Kuchukua tahadhari wakati wa kunyonyesha wakati wa janga hili la COVID-19

Kufikia sasa, hakuna ushahidi wowote wa virusi hivyo kupatikana katika maziwa ya mama kukifanya chakula salama zaidi kwa watoto wachanga. Kwa sababu hii, mama wanahimizwa kuendelea kunyonyesha watoto wao.

Wakati mama hupata COVID-19, kingamwili hutengenezwa katika maziwa yao kulinda mtoto wao na kuongeza kinga ya mtoto mwenyewe ndiposa kumnyonyesha ndio njia bora ya kulinda watoto wako dhidi ya virusi.

Tahadhari zaidi wakati wa kunyonyesha ili kuepusha kueneza virusi kwa watoto wao wachanga.

LINDA_MTOTO.png

Cha kufanya ili kuzuia kueneza COVID-19 wakati wa kunyonyesha:

  • Osha mikono na sabuni kabla na baada ya kumgusa mtoto.
  • Kuvaa barakoa ukiwa karibu na mtoto na wakati wa kunyonyesha
  • Kusafisha na kuua viini mara kwa mara
  • Wakati mama anaugua, anaweza kutumia kikombe na kijiko kulisha mtoto na maziwa ya mama au kumuuliza mtu aliye na afya bora kufanya hivyo wakati anachukua tahadhari zote zinazohitajika.
  • breastmilk or ask someone who is well to do it while taking all the necessary precautions.

Kuumpa mtoto vyakula vingine kunaweza kuwa hatari kwa watoto walio chini ya miezi 6

 

Akina mama wanahimizwa kutowapa watoto wao vyakula vingine au vimiminika kama fomula ya watoto wachanga, maziwa ya wanyama na maji kabla ya miezi 6. Hii inapunguza faida ambazo mtoto wako hupata kutoka kwa maziwa ya mama.

Katika miezi 6, mtoto bado ana mfumo wa mapema, kwa hivyo kumpa chakula au vinywaji kutaumiza tumbo. Pia itachukua nafasi ya kinga ya maziwa ya mama na kuwaacha katika hatari ya magonjwa ya kuambukiza kama COVID-19.

Hatari ya lishe mchanganyiko ni : -

  • Kuongezeka kwa hatari ya magonjwa ya utotoni kama kuhara na ugumu wa kupumua
  • Kuongezeka kwa hatari ya mtoto wako kupata magonjwa sugu kama unene kupita kiasi, magonjwa ya moyo baadaye maishani
  • Ugumu wa kuelewana na mtoto.
  • Inaweza kupunguza alama ya mtoto wako kwenye vipimo vya akili
  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata anemia, saratani ya ovari na saratani ya matiti

Tunapoadhimisha wiki ya Unyonyeshaji ya mwaka huu, Julisha.Info ingependa kuwakumbusha kuwa kunyonyesha ni jukumu la pamoja. Hakuna mtu anayepaswa kuachwa nyuma. Tuhimize kila mama anyonyeshe mtoto wake kwani hiyo ni zawadi ya thamani zaidi ambayo mama anaweza kumpa mtoto wake.   #WBW2021

Je, una maswali yoyote yanayohusiana na unyonyeshaji? Tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info, Jumatatu hadi Ijumaa kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni.