Jina RUTF ni maarufu sana. Utalisikia likitajwa hasa katika maeneo ambako watoto wanakumbwa na changamoto ya kukosa chakula cha kutosha au kutokula vyakula vinavyohitajika kwa miili yao kukua na kuishi kwa afya. Ikiwa unakutana na kifupi hiki RUTF kwa mara ya kwanza, makala hii itakusaidia kuelewa RUTF na jukumu lake katika kuokoa maisha ya watoto.

RUTF kwa kirefu ni Ready-to-Use Therapeutic Food (Chakula cha Tiba kilicho tayari kutumiwa). Ni bidhaa ya chakula iliyobuniwa kwa ajili ya kutibu na kudhibiti ukosefu wa lishe bora. Duniani kote, matumizi ya RUTF yamepata umaarufu mkubwa kama mbinu muhimu ya kutibu hali ya kudhoofika mwili na kupungua uzito kwa kiwango kikubwa (utapiamlo mkali wa muda mfupi) na kudhibiti utapiamlo wa wastani (utapiamlo wa wastani wa muda mfupi).

Utapiamlo wa muda mfupi ni hali inayotishia maisha. Husababishwa na mambo yafuatayo:

  • Kutokula chakula cha kutosha.
  • Magonjwa ya mara kwa mara yanayozidishwa na uhaba wa chakula au ukosefu wa chakula katika boma.
  • Mazoea duni ya malezi ya watoto.
  • Hali duni za maji, usafi, na mazingira.

Duniani kote, watoto ndio wanaoathirika zaidi. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), kufikia mwaka 2022, watoto milioni 45 walikuwa wakikabiliwa na hali ya utapiamlo wa kupungua uzito (wasting), ambapo milioni 13.7 walikuwa na utapiamlo mkali. Nchini Kenya, inakadiriwa kuwa idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6-59 wanaohitaji matibabu kwa ajili ya utapiamlo wa kupungua uzito itafikia 760,488 kufikia Januari 2025. Pia, inatarajiwa kuwa idadi ya wanawake na wasichana wajawazito au wanaonyonyesha wanaohitaji matibabu kwa utapiamlo mkali itafikia 112,401 kufikia Januari IPC July 2024-Jan 2025  

Ni changamoto hii ambayo RUTF imeundwa kushughulikia. Katika kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab, huduma za lishe zinazotolewa na Shirika la International Rescue Committee (IRC) hutegemea RUTF zinazotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF). RUTF hutolewa ili kusaidia kupunguza vifo vya watoto na kuboresha viwango vya kupona kwa watoto wenye utapiamlo.

Kuelewa Utapiamlo dhidi ya Kupungua Uzito (Wasting)

  • Utapiamlo ni hali ambapo mwili hauna virutubisho vya kutosha (utapiamlo duni) au una virutubisho zaidi ya vinavyohitajika (utapiamlo wa ziada). Ni neno linalojumuisha hali nyingi zinazohusiana na ulaji wa chakula.
  • Kupungua uzito (Wasting) ni hali ya kuwa na uzito mdogo ukilinganisha na urefu wa mtu. Mara nyingi, inaashiria kupoteza uzito kwa haraka na kwa kiwango kikubwa, ingawa inaweza pia kudumu kwa muda mrefu. Hali hii hutokea pale mtu anapokosa chakula bora na cha kutosha, na/au pale ambapo mtu anakumbwa na magonjwa ya mara kwa mara au ya muda mrefu. Kwa watoto, kupungua uzito kunaambatana na hatari kubwa ya kifo ikiwa haitatibiwa ipasavyo.

Kupungua uzito huainishwa kama kali, wastani, au hakuna kupungua uzito. Ili kutathmini na kuainisha hali ya kupungua uzito, mbinu tatu za vipimo hutumika, kama ilivyoainishwa hapa chini:

 

1.Alama za Uzito kwa Urefu (Weight for Height Z-scores - WHZ)

  • Kipimo hiki hutathmini hali ya unene kwa mtoto kwa kutumia uzito na urefu wake.

weight.jpg       height.jpg

Mashine za Kupima Uzito wa Mtoto na Urefu  Picha/Irene Njiru

2.Kipimo cha Mzunguko wa Juu wa Mkono (Mid-Upper Arm Circumference - MUAC)

  • Laini za MUAC hutumika hasa kupima mzunguko wa juu wa mkono wa watoto na pia wanawake wajawazito ili kubaini visa vya utapiamlo.
  • Rangi Nyekundu: Inaonyesha kuwa mtoto ana utapiamlo mkali na anapaswa kupelekwa hospitalini kwa matibabu mara moja.
  • Rangi ya Njano: Inaonyesha kuwa mtoto ana utapiamlo wa wastani na anapaswa kupelekwa hospitalini ili kupata virutubishi vya ziada kama vile Plumpy Sup.
  • Rangi ya Kijani: Inaonyesha kuwa mtoto ana lishe bora.

muac real.png  

 Kwa Hisani ya UNICEF: Mfano wa Laini ya MUAC.

blobid0.png

Mtoto Akipimwa kwa Kutumia Laini ya MUAC. Chanzo cha Picha: UNICEF/UNI494305/Moran

3.Edema-Hali ambapo mwili huvimba kutokana na ukosefu wa virutubisho muhimu, hasa protini. Kuvimba huku kunatokana na maji mengi yanayokusanyika kwenye tishu za mwili. Hali hii huonekana mara nyingi kwenye miguu, mguu wa chini, au usoni. 

blobid1.png

Uvimbaji (Edema) kwenye Miguu Miwili  Chanzo cha Picha: Valid International2018

Chakula cha Tiba Kilicho Tayari Kuliwa (RUTF) kinaweza kutumika kutibu utapiamlo wa kupungua uzito wa kiwango cha kali na wastani

Nini kinachotumika kutengeneza RUTF?

rutf-Landscape.jpg

Mfano wa Pakiti ya RUTF Picha/Irene Njiru

RUTF au “chakula cha tiba kilicho tayari kutumiwa”, ni unga inayookoa maisha yenye nishati na virutubisho vingi. Hutengenezwa kwa njugu, sukari, maziwa ya poda, mafuta, vitamini na madini na hutumika kutibu utapiamlo wa kupungua uzito kwa watoto chini ya miaka 5. Kila pakiti ya RUTF ina kalori 500 na virutubisho vidogo (micronutrients) vyenye:

  • Thamani kubwa ya lishe inayowawezesha watoto au watu wazima wenye utapiamlo kuongeza uzito haraka. Ina rafu ya miaka miwili, na kufanya iwe rahisi kuhifadhi kwenye ghala.
  • Ladha inayovutia na urahisi wa .
  • Haitaji maandalizi – watoto au watu wazima wanaweza kula moja kwa moja kutoka kwenye pakiti.
  • Ina nishati nyingi na virutubisho vingi; pia ina chuma.
  • Uwezo wa kurekebisha hali ya lishe ya watoto walio na utapiamlo mkali chini ya miaka 5.

Jinsi ya Kutumia RUTF Wakati wa Matibabu

  • RUTF ni dawa maalum ya kutibu utapiamlo wa wastani na utapiamlo mkali wa muda mfupi na imetengenezwa kukidhi mahitaji maalum ya lishe ya watoto wenye utapiamlo.
  • Haitakiwi kugawanywa na watu wengine wa familia walio na afya njema.
  • Kula RUTF mara kwa mara ukiwa na afya nzuri kunaweza kuleta madhara, ikiwa ni pamoja na kuongezeka uzito, usawa wa virutubisho, matatizo ya ‘digestion’ wa chakula na kupoteza hamu ya kula vyakula vya kawaida. Watoto wanapaswa kula RUTF TU pale ambapo daktari ameshauri.
  • Kwa watoto wanaonyonyesha, inashauriwa mama awape maziwa ya mama kwanza kabla ya RUTF.
  • RUTF inapaswa kulwa kabla ya vyakula vingine, toa milo midogo ya RUTF kwa wakati unaofaa na mhamasishe mteja (au mtoto) kula kwa masaa 3-4.
  • wakati wa kula RUTF inapaswa mtoto/mteja kunwa na maji mengi
  • Mtunzaji anapaswa kutumia sabuni na maji yanayotiririka ili kusafisha mikono yao na mtoto kabla ya kumlisha.
  • Hakikisha pakiti za RUTF ziko safi na zimefunikwa.
  • Chunguza mtoto wako kwa matatizo kama vile kuhara, kutapika, na ikiwa wanamaliza rations za kila wiki na ripoti ya maendeleo kwa hospitali au mtoa huduma aliyependekeza RUTF.
  • Ikiwa mtoto wako hakuli, anapungua uzito, kutapika, kuongezeka au kukuwa na edema, kuwa na kuhara au mgonjwa, nenda kwa kituo cha afya kwa matibabu na ushauri.
  • Hakikisha unamleta mtoto wako kwa kituo cha afya kila wiki kwa uchunguzi na kupokea usambazaji wa RUTF.
  • Kwa RUTF iliyotolewa na IRC, rudisha pakiti za RUTF tupu unapoenda kwenye kituo cha afya kwa uchunguzi wa kila wiki.

Uuzaji au Ununuzi wa RUTF Sokoni au Dukani

Uuzaji wa RUTF unakatazwa vikali. Ikiwa bidhaa hizi za lishe zitapatikana sokoni, inamaanisha kuwa mtoto au mteja aliye na hitaji la dharura la lishe inayookoa maisha alikosa dawa hii.

Huduma za Lishe katika Kambi

Huduma za lishe zinapatikana katika vituo vya afya nchini Kenya. Katika kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab, huduma za lishe zinatolewa na mashirika matatu:

  • IRC (Kakuma, Hagadera)
  • KRCS (Ifo, Ifo 2, Kalobeyei)
  • MSF (Dagahaley).

IRC inatoa huduma za lishe katika vituo vyote bila malipo. Angalia huduma hizi hapa:

Kituo cha AfyaHuduma zinazopatikanaMawasiliano
Dadaab Sub-County Hospital Lishe bora 

simu: 254717057288

254725079404

Amusait General Hospital (The IRC General Hospital) - Kakuma Huduma ya lishe 

simu

254701629346

Kaapoka Health Centre (The IRC Main Hospital) Nutrition  simu: 254701629345
Hong Kong Dispensary (Clinic 2-IRC) Huduma ya Lishe   
Nationakor Dispensary (Clinic 6-IRC) Nutrition  simu: 254701629346
International Rescue Committee (IRC) - HagaderaHuduma za Lishe na Afyasimu: 0800720143

 

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820) ,Jumatatu hadi Ijumaa kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni.