Saratani ya mlango wa tumbo la uzazi (Cervix)ni saratani inayoanzia kwenye mlango wa tumbo la uzazi wa mwanamke. Mlango wa tumbo la uzazi (cervix) ni ufunguzi wa mfuko wa uzazi (uterus). Inaunganisha uke (au njia ya uzazi) na tumbo la uzazi. Virusi vya Human papillomavirus (HPV), maambukizi ya kawaida ya zinaa, ni sababu kuu ya saratani ya mlango wa tumbo la uzazi. Lakini sio maambukizo yote ya HPV yanayo sababisha saratani ya tumbo la uzazi. Saratani ya hii kwa kawaida huanza na mabadiliko kwenye seli ya tumbo la uzazi, inayoitwa dysplasia. Seli hizi zisizo za kawaida zinaweza kuondolewa ili kuzuia saratani ikiwa itapatikana mapema.

Dalili za saratani ya mlango wa tumbo la uzazi ni zipi?

Saratani ya mlango wa tumbo la uzazi ikianza, mara nyingi haina dalili. Kadiri mwanamke anavyoendelea kuugua saratani yhii bila matibabu, ndivyo uwezekano wake kuwa na dalili. Baadhi ya dalili za a baadaye za saratani hii zinaweza kujumuisha:

  • Kutokwa na damu nyingi ukeni au usaha (zaidi ya kawaida)
  • Kutokwa na damu baada ya kujamiiana, katikati ya hedhi au baada ya uchunguzi wa fupanyonga (pelvic exam)
  • Maumivu wakati wa kujamiiana au kuenda haja ndogo

Ikiwa una mojawapo ya dalili hizi, tembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe. Dalili hizi zinaweza kusababishwa na kitu kingine, lakini njia pekee ya kujua kwa uhakika ni kumuona mhudumu wako wa afya.

Je, ni mambo gani yanayoongeza hatari ya mtu kupata saratani ya mlango wa tumbo la uzazi?

Hatari ni kitu chochote kinachoongeza uwezekano wa kupata ugonjwa. Mwanamke yeyote anaweza kupata saratani ya mlango wa tumbo la uzazi, lakini baadhi ya wanawake wako kwenye hatari zaidi kwa sababu ya mambo kama vile:

  • Kuwa na Virusi vya Human Papillomavirus (HPV)

HPV husababisha takriban visa vyote vya saratani ya mlango wa tumbo la uzazi. Ni maambukizi ya kawaida ya zinaa. Wanaume na wanawake wanaweza kuwa na HPV.

HPV mara nyingi huenda yenyewe, lakini ikiwa haifanyi hivyo, inaweza kusababisha saratani ya mlango wa tumbo la uzazi kwa wanawake. Wanawake wengi hupata maambukizi ya HPV wakati fulani katika maisha yao, lakini wachache watapata saratani ya mlango wa tumbo la uzazi.

  • Kutochunguzwa

Saratani ya mlango wa tumbo la uzazi mara nyingi hupatikana kwa wanawake ambao hawajachunguzwa (kupimwa au kuchunguzwa). Uchunguzi wa saratani hutafuta saratani kabla ya kuwa na dalili zozote. Saratani iliyopatikana mapema inaweza kuwa rahisi kutibiwa.

Unapopimwa, wahudumu wa afya wataangalia uwepo wa seli zisizo za kawaida au maambukizi ya HPV. Wanawake ambao wamefanyiwa uchunguzi lakini hawafuatilii wahudumuwao wa afya wakati matokeo yanapotoka yasiyo ya kawaida pia wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya mlango wa tumbo la uzazi.

  • Kuvuta sigara

Wanawake wanaovuta sigara wana uwezekano wa mara mbili zaidi wa kupata saratani ya mlango wa tumbo la uzazi, ikilinganishwa na wanawake ambao hawavuti sigara.

Utafiti unaonyesha kuwa sigara inaweza kuharibu seli za mlango wa tumbo la uzazi, hali ambayo inaweza kusababisha saratani. . Uvutaji sigara pia hudhoofisha kinga ya mwili, na kuifanya kuwa ngumu kupigana na maambukizi ya HPV.

  • Umri

Wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 30 wana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya mlango wa tumbo la uzazi.

Sababu zingine zinazoongeza hatari ya kupata saratani ya mlango wa tumbo la uzazi ni pamoja na:

  • Ikiwa umetibiwa saratani ya mlango wa tumbo la uzazi, au kwa kuwa na seli zisizo za kawaida ambazo zinaweza kuwa saratani
  • Kujifungua mara tatu au zaidi
  • Kuwa na wapenzi wengi inakuweka kwa hatari ya kupatavirusi vya HPV ambayo ndiyo sababu kuu ya saratani ya mlango wa tumbo la uzazi
  • Kuwa na Virusi vya Ukimwi (HIV), virusi vinavyosababisha UKIMWI, au hali nyingine yoyote ambayo inafanya kuwa vigumu kwa mwili wako kupigana na maambukizi.

Je, ninawezaje kupunguza uwezekano wangu wa kupata saratani ya shingo ya kizazi?

Cervical Cancer Article -swahili.png

Sababu zingine za hatari, kama vile umri, haziwezi kudhibitiwa, lakini zingine zinaweza. Baadhi ya njia za kupunguza hatari ya kupata saratani ya mlango wa tumbo la uzazi au kuizuia kabisa ni:

  • Pata Chanjo

Chanjo ya HPV hulinda dhidi ya aina za HPV ambazo mara nyingi husababisha saratani ya mlango wa tumbo la uzazi. Inapendekezwa kwa wanaume na wanawake.

Kwa wanawake, chanjo ya HPV husaidia kuzuia saratani ya mlango wa tumbo la uzazi, na uke. Pia hulinda dhidi ya saratani ya njia ya haja kubwa, mdomo na koo. Chanjo hiyo hutolewa kwa wasichana wenye umri wa miaka 9-11.

  • Kaguliwa

Saratani ya mlango wa tumbo la uzazi inaweza kuzuilika au kupatikana mapema kwa uchunguzi wa mara kwa mara. Kuna kipimo kimoja cha uchunguzi ambacho kinaweza kusaidia kuzuia saratani yhii au kuipata mapema:

Ukaguzi wa Macho kwa kutumia asidi ya asetiki

Kwa hili, mhudumu wa afya atajadiliana nawe kuhusu uchunguzi kisha kifaa kinachoitwa "speculum" kitaingizwa kwa uangalifu ndani ya uke ili kufungua shingo la uzazi. Kisha asidi ya asetiki huwekwa kwenye mlango wa tumbo la uzazi na kuchunguzwa kwa mabadiliko ya rangi. Iwapo itabadilika kuwa chanya (Positive), matibabu hufanywa papo hapo na ikiwa hasi(negative), utapewa kadi (Biodata, nambari ya kipekee uliyopewa, usawa, ishara muhimu (usomaji wa shinikizo la damu) aina ya uchunguzi uliofanywa na matokeo na tarehe ya kurudi

Mapendekezo ya Uchunguzi wa Saratani ya mlango wa tumbo la uzazi kwa Wanawake walio katika Hatari ya Wastani

  • Wanawake wenye umri wa miaka 18 hadi 65 wana chaguo la kuchunguzwa kila baada ya miaka 5
  • Wanawake ambao hawafashiriki ngono au wanaofikiri kuwa miaka kao ya kupata watoto imekwisha bado wanapaswa kuchunguzwa mara kwa mara kwa saratani ya mlango wa tumbo la uzazi.
  • Wanawake ambao wamepata chanjo ya HPV bado wanahitaji uchunguzi wa mara kwa mara.
  • Wanawake wanaweza kuacha kuchunguzwa ikiwa wana zaidi ya miaka 65 na wamekuwa na matokeo ya uchunguzi wa kawaida kwa miaka 10.
  • Wanawake ambao wameondolewa seviksi wakati wa upasuaji kwa sababu zisizo za kansa, kama vile fibroids, wanaweza wasihitaji kuchunguzwa.

Ninaweza kupata wapi uchunguzi wa saratani ya mlango wa tumbo la uzazi?

Uchunguzi wa saratani ya mlango wa tumbo la uzazi unapatikana bila malipo katika vituo vyote vya IRC huko Kakuma na hospitali kuu ya Hagadera.

Je, ninaweza kupata matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi?

NDIYO.I Ikiwa saratani hiyo imegunduliwa mapema.

 

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820) ,Jumatatu hadi Ijumaa kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni.