Coronavirus husababisha ugonjwa wa kuambukiza wenye dalili tofauti, kutoka kwa dalili dhaifu hadi ugonjwa mbaya. Dalili zinaweza kuonekana kati ya siku 2 hadi 14 baada ya kuambukizwa. Watu walio na dalili zifuatazo wanaweza kuwa na ugonjwa wa COVID-19:

 • Joto
 • Kukohoa
 • Shida ya kupumua.
 • Uchovu
 • Maumivu ya misuli na mwili
 • Kuumwa na kichwa
 • Upotevu mpya wa hisia za wa kunusa na kuonja chochote (Upotevu wa ladha na harufu)
 • Kuumwa na koo
 • Homa
 • Kichefuchefu au kutapika
 • Kuhara

Ishara_na_dalili.png

Hizi ni dalili za mara kwa mara, lakini orodha hii haijumuishi dalili zote zinazowa kupatikana.

Unashauriwa kutembelea kituo cha afya au hospitali iliyo karibu na wewe unapohisi jambo lisilo la kawaida.

Ukiwa Kakuma unaweza kutembelea:

KITUO

ENEO

Kituo cha Afya cha Kaapoka (Main Hospital)

Kakuma 1

Kliniki ya Lochangamor (Clinic 4)

Kakuma 1

Kliniki ya Hong-Kong (Clinic 2)

Kakuma 2

Kliniki ya Nalemsekon (Clinic 5)

Kakuma 2

Kliniki ya Nationokor (Clinic 6)

Kakuma 3

Hospitali ya Jumla ya Ammusait (IRC General Hospital)

Kakuma 4

Kituo cha Afya cha Natukubenyo (Kalobeyei Health centre)

Kalobeyei V1

Kliniki ya Naregae (Kalobeyei Village 2 Clinic)

Kalobeyei V2

 

 

Ukiwa Dadaab, unaweza kupiga simu kwa mashirika yafuatayo kwenye nambari za usaidizi za bure:

 

KITUO

ENEO

Red Cross

Kambi ya Ifo

Kambi ya Dagahaley 

Hagadera refugee camp hospital

Kambi ya Hagadera

Ikiwa:

 1. Umepimwa na ukapatikana kuwa na ugonjwa wa COVID-19 lakini huna dalili zozote za ugonjwa huo, ama
 2. Una dalili za COVID-19 lakini hauhitaji kulazwa hospitalini,

Unafaa kujitenga na watu ili  kuwakinga watu wengine, kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya kutoka Wizara ya Afya nchini Kenya na Shirika la Dunia la Afya (WHO).

Hii inamaanisha kuwa utajitenga na wengine, hata nyumbani mwako.

 • Ikiwezekana, kaa katika chumba tofauti na watu wengine. Tumia bafu/choo tofauti,
 • Tumia viombo vya kibinafsi (kama vikombe, taulo, na dawa ya meno) na usitangamane na wengine.
 • Kula mbali na watu unaoishi nao.

Ikiwa ulikaribiana na mtu ambaye tayari ameambukizwa na ugonjwa wa COVID-19, unafaa kuenda karantini. Katika kujiweka karantini, wataalum wa afya wanapendekeza ukae mbali na watu kwa siku 14 kuona kama dalili za ugonjwa zitatokeza.

Hii ni kwa sababu:

 1. Unawezakuwa kuwa umeambukizwa virusi na hujui, au
 2. Unaweza kuwa umeambukizwa ugonjwa wa COVID-19 lakini huonyeshi dalili zozote.

Karantini inasaidia kuzuia uenezaji wa COVID-19

Nitafanya nini nikipimwa na kupatikana kuwa nina ugonjwa wa COVID-19  lakini sina dalili, au nina dalili dhaifu?

Iwapo utapimwa na upatikane kuwa na ugonjwa wa COVID-19 na una dalili dhaifu za ugonjwa huo, wataalamu wa afya wanapendekeza kuwa upate matibabu nyumbani.  Hii inahusisha:

 • Kusalia nyumbani kwa siku 10.
 • Kuvaa barakoa wakati wote – Unaweza kununua barakoa kutoka duka lililo karibu nawe.
 • Kama inawezekana, jitenge na watu unaoishi nao
 • Mteue mtu atakayekusaidia kununua vitu dukani na sokoni, na atakaye kukusaidia kuchota maji au kazi zingine za nyumbani kama kupika
 • Kohoa ama upige chafya kwenye kiwiko cha mkono wako, ama ufunike mdomo wako na kitambaa ama unapokohoa ama kupiga chafya kisha utupe kitambaa ama tishu kwenye pipa au kwenye choo.
 • Usitumie vitu vya kibinafsi vya nyumbani, kama vikombe, taulo, na vyombo na watu wengine.
 • Nawa mikono kutumia sabuni na maji kwa angalau sekunde 20. Iwapo sabuni na maji hazipatikani, tumia sanitiza za vileo isiyopungua 60%.

Msaidizi wa Afya ya kijamii  atakutembelea nyumbani kila siku kufuatilia hali yako ya afya, kama unaishi katika kambi za Kakuma au Hagadera.

mceclip0.png

Picha/Kenneth Mwenda

Ni muhimu uwe mtulivu wakati huu wa kutengwa. Watu wengi wanaopata COVID-19 wana dalili dhaifu za ugonjwa huo na hupona bila kuhitaji kulazwa hospitalini. Unapaswa pia kujaribu kutangamana na watu kwani hii itapunguza hatari ya kuwaambukiza wengine.

Nitafanya nini ikiwa nimekaribia mtu aliye na ugonjwa wa COVID-19, ama nimekuwa karibu na mtu aliyepatikana kuwa na ugonjwa wa COVID-19?

 • Kaa nyumbani kwa siku 14 baada ya mara ya mwisho ya kuwa kwenye hatari ya kuambukizwa. Unaweza maliza karantini yako baada ya siku 10 iwapo hauna dalili zozote za ugonjwa huo. Hata hivyo, unashauriwa kufuatilia dalili zako hadi siku 14 ziishe.
 • Kuwa macho kubaini dalili. Angalia homa, kikohozi, matatizo ya kupumua au dalili zingine za COVID-19.
 • Hakikisha hutangamani na watu: jaribi iwezekanavyo kuweka umbali wa angalau mita moja (futi 3) kati yako na watu wengine.
 • Kaa mbali iwezekanavyo na watu wengine. Vaa barakoa unapokuwa karibu na watu.
 • Hakikisha kuwa hutangamani na watu nyumbani iwapo una dalili za COVID-19. Tafuta ushauri wa  ikiwa dalili zinazidi kuwa mbaya.

Tafuta ushauri wa daktari iwapo:

 • Dalili zako zinazidi kuwa mbaya na haujapata nafuu baada ya siku 7.
 • Ikiwa umechanganyikiwa
 • Ikiwa unapata joto upya, ama joto kuongezeka mwilini
 • Ukipata maumivu ya kifua
 • Ikiwa unashindwa kupumua, na unapumua zaidi ya mara 25 ndani ya dakika moja.

Vitu vya kuepuka unapokuwa karantini ama unapojitenga.

 • Usitoke nyumbani
 • Usiende  kazini
 • Epuka mikusanyiko ya watu kama vile makanisa na misikiti, mikutano ya hadhara, vituo vya kijamii, maduka, harusi, mazishi, na vituo vya usambazaji wa chakula, kati ya maeneo mengine
 • Usimtembelee yeyote
 • Usiwe na wageni wowote nyumbani
 • Usiondoke nyumbani, isipokuwa unapo hitaji matibabu
 • Karantini inatumika kumweka mtu ambaye anaweza kuwa ameambukizwa COVID-19 mbali na wengine, ilhali Kujitenga kunatumika kuwatenganisha watu walioambukizwa na virusi (wale ambao ni wagonjwa na wale wasio na dalili) na watu ambao hawajaambukizwa.

Symptoms_in_Swahili.png

Kwa maelezo zaidi, ama iwapo  unamjua mtu mwenye dalili za ugonjwa wa COVID-19, piga simu kwa 719 ama bonyeza *719#. Kumbuka hizi ndizo nambari rasmi zilizotolewa na Serikali ya Kenya.

Unaweza pia kupiga simu kwa nambari zifuatazo:

 • Nairobi                       0800721316 (Haina Malipo) / 0732353535
 • Kambi ya Ifo               0726368506/0725942928
 • Kambi ya Dagahaley  0795759743
 • Hagadera, Garissa      0800720143/ 0111207207 / 0110040836 / 011040708
 • Kakuma, Turkana       0758722023/ 0800720605                    

Tungependa pia kukukumbusha kuhusu nambari unazoweza piga wakati wa dharura.

 • Nambari ya simu ya Kitaifa ya Ukatili wa Kijinsia : 1195
 • Nambari ya simu ya dharura ya polisi Kenya: 999/112
 • Nambari ya simu ya shirika la MSF (Madaktari wasio na mipaka) ya ukatili wa kijinsia: 0711400506
 • Shirika la Afya ya LVCT (Ushauri wa hiari wa Liverpool na matibabu ya Virusi vya Ukimwi): 0800720121

Iwapo una maswali yoyote, wasiliana nasi kupitia ukurasa wa Julisha.Info kwenye mtandao wa Facebook, kila Jumatatu hadi Jumamosi kutoka saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.