Ikiwa unaishi katika Kambi za Wakimbizi za Dadaab au Kakuma na unahitaji chanzo cha habari cha kuaminika, redio ni chaguo nzuri kupata habari zinazoweza kuokoa maisha.

Unaweza kujiunga na 'Bilan' na 'Sauti ya Mwanamke', vipindi viwili vya redio vinavyoundwa na kutangazwa na shirika la kimataifa la Internews.

Vipindi hivi viwili vya redio vinashiriki habari za kuaminika zinazotolewa kwa wakati unaofaa, na zinazoweza kuokoa maisha kwa watu wanaoishi Kakuma na Dadaab.

Je! Vipindi hivi vya Redio vimeundwa vipi?

Ikirushwa hewani kupitia mitabendi 90.1 FM huko Kakuma na Kalobeyei, mitabendi 97.1 / 2 FM huko Dadaab, na mitabendi 105.9 Star FM huko Nairobi, kipindi hicho ni kipindi cha mazungumzo kinachorushwa moja kwa moja na kinasimamiwa na mtangazaji wa kike kutoka kwa jamii husika.

Wasikilizaji hupiga simu na kutoa maoni yao kuhusu mada zinazojadiliwa. Mtangazaji wa kipindi hicho pia husoma maoni ya wasikilizaji na huruhusu mtaalam au wataalam waliopo studio wakati wa kipindi hicho kutoa majibu na maoni yao.

Rose_Internews.jpg

Rose Kapengi wa Radio Atta Nayece, akisimamia kipindi katika studio za redio ya jamii huko Kakuma mnamo Novemba 2020. Picha imechukuliwa na Stellar Murumba @Internews.

Huko Kakuma, kipindi hicho kinarushwa moja kwa moja kutoka saa 1:30 jioni hadi 2:30 jioni kila Jumamosi, kisha rekodi ya kipindi hicho huchezwa masaa kama hayo Jumapili.  Huko Dadaab na Nairobi, kipindi hicho kinarushwa moja kwa moja kutoka saa 5 asubuhi hadi saa 6 mchana kila Jumamosi, na rekodi ya kipindi hicho hurushwa tena masaa kama hizo Jumapili.

Kipindi hicho kina wanajopo kutoka sehemu mbali mbali za Maisha, wakiwemo wakimbizi, wanaotafuta hifadhi, jamii zinazotoa hifadhi kwa wakimbizi, wataalam wa maswala ya wakimbizi, wafanyikazi wa mashirika inayotoa misaada ya wakimbizi, maafisa wa serikali, madaktari, na wanasheria.

 

Maoni

Wasikilizaji hupiga simu wakati kipindi cha moja kwa moja kinaporushwa, na kutuma maswali na maoni kupitia ujumbe wa SMS na mitandao ya kijamii; kisha wanajibiwa hewani na wanajopo.

  • Ukiwa Kakuma and Kalobeyei, tuma maoni kwa Radio Atta Nayece kupitia ujumbe wa SMS kwa nambari 0799870868
  • Ukiwa Nairobi and Dadaab, tuma maoni kwa Star FM na Radio Gargaar kwa namba 22960.

Vituo hivyo vya redio pia hupaikana kwenye mitandao ya kijamii na huchapisha mara kwa mara kwenye mitandao ya Facebook na Twitter.

Iwapo una maswali yoyote, wasiliana nasi kupitia ukurasa wa Julisha.Info kwenye mtandao wa Facebook, kila Jumatatu hadi Jumamosi kutoka saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.