Ugonjwa wa COVID-19 unasababishwa na virusi vya SARS-CoV-2, ambao unasambaa kati ya watu, haswa mtu aliye na ugonjwa huo akitangamana kwa karibu na mtu asiye na ugonjwa huo.

Virusi hivyo vinaweza kusambaa kupitia mdomo ama pua la mtu aliye na ugonjwa huo anapokohoa, anapopiga chafya, anapozungumza, anapoimba, ama anapopumua kwa nguvu. 

Tazama video hii kuelewa kuhusu ugonjwa wa COVID-19 nchini Kenya.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza kuchukua hatua zifuatazo ili kujikinga na kuikinga familia zetu dhidhi ya ugonjwa wa COVID-19:

  • Kaa umbali wa angalau mita moja mbali na watu wengine.
  • Vaa barakoa unapotoka nje, na ikiwa huwezi kukaa umbali wa mita moja kutoka kwa watu wengine.
  • Epuka mahali penye mikusanyiko ya watu. Punguza ukubwa wa mikusanyiko, iwe kwa muda mfupi, na ifanyike nje kama inawezekana
  • Fungua madirisha ukiwa ndani ya nyumba ili kuhakikisha kuwa kuna hewa ya kutosha.
  • Epuka kugusa nyuso zinazoguswa mara kwa mara kama vile meza, viti, vitasa vya milango, swichi za taa, rimoti, vidude vya kuchezea watoto, na vyoo, mara kwa mara. Ikiwezekana, safisha nyuso hizo mara kwa mara.
  • Nawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20, ama kwa kutumia “sanitizer” iliyo na kiwango cha kileo cha asilimia 60.
  • Funika mdomo na pua unapokohoa na upige chafya kwenye kwiko lako. Tupa karatasi za shashi zilizotumika kisha unawe mikono yako.
  • Kaa nyumbani na mbali na watu wengine ukiwa na dalili kama kikohozi, kupiga chafya na homa.

Tazama video hii ili kujua dalili za COVID-19 na hatua za kuchukua ili kujikinga na ugonjwa huo.

Kwa maelezo zaidi, ama iwapo wewe ama mtu unayemjua ana maumivu, homa ama anakohoa, piga 719 ama bonyeza *719#. Hii ni nambari ya dharura iliyotolewa na Serikali ya Kenya.

Jikinge, ikinge familia yako, na ikinge jamii yako.

Iwapo una maswali yoyote, wasiliana nasi kupitia ukurasa wa Julisha.Info wa mtandao wa Facebook, kila Jumatatu hadi Jumamosi kutoka saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.