Service Image

Imesasishwa saa: 2023/09/26

SIKIKA inatoa ukwaa la taarifa na mawasiliano Kakuma, Kalobeyei, na jamii inayowakaribisha wakimbizi katika eneo hilo. Vikundi vya Wasikilizaji 290 wanapokea programu ya sauti ya dakika 30-45 kila wiki ,ambayo inatengenezwa na wakimbizi na wenyeji.  

SIKIKA inashughulikia mada zifuatazo na nyinginezo: 

 • Afya 
 • Usafi wa Mazingira 
 • Ulinzi 
 • Elimu 
 • Michezo 
 • Hadithi za Mafanikio 
 • Mazingira/Hali ya Hewa/Mabadiliko ya Tabianchi 
 • Makazi 
 • Chakula/Lishe 
 • Kilimo 
 • Tangazo la Huduma za Umma 
 • Haki za Wakimbizi 
 • Usalama na Ulinzi  

Vigezo vya Kustahiki

 • Kila mkimbizi,mwanachama wa jamii ya wenyeji wanaweza kujiunga na Kikundi cha Kusikiliza SIKIKA

Jinsi Huduma Zako Zinavyopatikana Ili kuwa mwanachama wa Kikundi cha Kusikiliza

 • Tafadhali wasiliana na Kiongozi wa Kikundi cha Kusikiliza katika eneo lako.  

Eneo

 • SIKIKA ina Vikundi vya Wasikilizaji kote Kakuma, Kalobeyei, na maeneo ya jirani. Ofisi iko Kakuma, kiwanja cha 3.  

Mifumo ya Maoni ya Taasisi na Masaa ya Kazi

 • Baada ya kila kikao cha kusikiliza, vikundi hujadili programu na maudhui. Wanawasilisha maoni kwa chumba cha wahariri cha SIKIKA ambapo yanachambuliwa na kipindi kipya kinatengenezwa kulingana na maoni hayo. 

Maelezo ya Mawasiliano

Anwani

Kakuma, Kenya

3.7090661
34.8624838

Bonyeza hapa kuona anwani katika Ramani za Google.