Malaria ni tishio kubwa la kiafya katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma. Katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2023, kulikuwa na zaidi ya kesi 23,000 za malaria na vifo 25 katika kambi hiyo.Wakimbizi na wanaotafuta hifadhi katika kambi wana uwezekano mkubwa wa kupata malaria. Hii ni kwa sababu watu wengi wanaishi pamoja kwa karibu, maji mengi yaliyosimama ambapo mbu huzaliana, na kukosa dawa za kutosha au wahudumu wa afya kuweza kutunza idadi ya watu ipasavyo. Pia hawana pesa za kununua vitu kama vyandarua ili kujikinga na kuumwa na mbu.

Mashirika kama vile International Rescue Committee (IRC) yanajitahidi kupunguza mzigo wa malaria katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma kwa kutoa huduma za matibabu na hatua za kuzuia.

Soma makala haya kuhusu dalili za malaria, jinsi ya kuzuia malaria na mahali pa kupata matibabu ya malaria katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma na makazi ya Kalobeyei.

 

Malaria inasababishwa na nini?

Malaria ni ugonjwa unaoenezwa na mbu. Mbu hupata malaria kutoka kwa watu walioambukizwa na hueneza kwa wengine wanapouma. Vimelea vinavyosababisha malaria huishi katika damu ya watu.

 

Dalili za Malaria

Dalili za malaria kwa kawaida huonekana ndani ya siku 10 hadi 15 baada ya kuumwa na mbu.

Dalili za malaria ni:

  • Homa kali
  • Baridi
  • Kuumwa na kichwa
  • Maumivu ya misuli
  • Uchovu
  • Kichefuchefu na kutapika

SWA.png

Malaria isipotibiwa inaweza kusababisha matatizo makubwa kama vile upungufu wa damu, malaria ya ubongo, ini na figo kushindwa kufanya kazi vizuri, kifafa, kuharibika kwa ubongo, kupoteza fahamu hata kifo, hasa kwa watu walio hatarini kama vile wanawake wajawazito, watoto, wazee na wale walio na ugonjwa zingine za kukandamiza kinga kama vile ukimwi, lupus, ugonjwa wa kisukari cha aina ya 1 na mengineyo.

 

Je, Malaria inatibika?

Ndiyo, Malaria inatibika. Ikiwa matibabu imefanywa kwa haraka na madhubuti, maambukizi yanaweza kuponywa, dalili zinaweza kupungua na idadi ya watu wanaougua au kufa kutokana na malaria inaweza kupunguzwa.

Ikiwa unashuku kuwa una malaria au unaonyesha dalili kama za malaria, unapaswa kutembelea hospitali au zahanati yoyote iliyo karibu nawe kwa uchunguzi na matibabu.

Unaweza kutembelea vituo vya afya vifuatavyo katika Kambi ya Wakimbizi ya Kakuma na Makazi ya Kalobeyei. Upimaji na matibabu katika vituo hivi ni bure. Hakikisha umebeba kitambulisho chako kama vile uthibitisho wa usajili au kitambulisho cha mkimbizi ikiwa wewe ni mkimbizi na kitambulisho cha kitaifa kwa wakenya unapotembelea kituo cha afya.

 

Kambi ya wakimbizi ya Kakuma

Kituo cha afyaMahaliSaa za kazi

Locher Angamor Dispensary (Kliniki ya nne)

Kakuma 1, Zone 1, Block 9, kando ya uwanja wa mpira wa kikapu  Kakuma 1Jumatatu – Jumamosi (8am – 3pm)

Kaapoka Health Centre (Hospitali kuu)

Kakuma 1, Zone 2, Block 15, kando ya kituo cha mafunzo cha Don BoscoJumatatu – Jumamosi (8am – 3pm)

Hong Kong Dispensary (Kliniki ya pili)

Kakuma 1, Zone 4, Block 1, kando ya kituo cha polisi cha HongkongJumatatu – Jumamosi (8am – 3pm)

Nalemsekon Dispensary (Kliniki ya tano)

Kakuma 2, Zone 1, Block 6Jumatatu – Jumamosi (8am – 3pm)

Nationakor Dispensary (Kiliniki ya sita)

Kakuma 3, Zone 3, Block 1, kando ya kituo cha polisi cha Kakuma 3Jumatatu – Jumamosi (8am – 3pm)

Hospitali kuu ya Amusait

Kakuma 4, Zone 1, Block 1, kando ya soko eneo la Kakuma 4Kila siku (Saa 24)

 

Makazi ya Kalobeyei

Kituo cha matibabu cha Natukubenyo (Kituo cha matibabu cha Kalobeyei)

Kalobeyei Kijiji cha kwanzaKila siku (masaa 24)

Naregae Dispensary (Kliniki katika Kijiji cha pili cha Kalobeyei)

Kalobeyei Kijiji cha piliKila siku (8am – 3pm)

 

Maelezo ya huduma za afya yanaweza kupatikana kwenye ramani ya huduma ya Julisha.info:

https://www.julisha.info/hc/sw/sections/4403359499671-Kakuma?services=1558

Ili kuweza kutumia ramani ya huduma kwenye tovuti ya Julisha.Info, bonyeza eneo ilioandikwa "Ramani ya Huduma". Kutoka hapo, chagua eneo lako, ambalo linaweza kuwa Kaunti za Turkana, Garissa, au Nairobi. Baada ya kuchagua eneo lako, unaweza kuchagua eneo lako mahususi ili kuweza kuona huduma zinazopatikana katika eneo hilo.

Unaweza pata huduma mahususi kirahisi kwa kuchagua huduma unazohitaji kwa kubonyeza enao la "Huduma zote" kilicho kwenye sehemu ya juu ya kulia ya kompyuta au simu yako. Hii itakuruhusu kuzingatia huduma mahususi za afya unazohitaji.

Capture2.PNG

Kakuma: Huduma ya Afya - Kliniki ya Nationokor (Clinic 6) International Rescue Committee (IRC)

 

Je, tunawezaje kuzuia maambukizi ya Malaria?

Ili kukomesha kuenea kwa malaria, tunahitaji kudhibiti mbu na kuwasaidia watu kujikinga. Hapa kuna baadhi ya mikakati muhimu:

  • Kulala chini ya neti iliyotibiwa: Hii husaidia kujikinga dhidi ya kuumwa na mbu, hasa wakati wa kulala.
  • Unyunyiziaji wa dawa za kuzuia wadudu dhidi ya malaria: Utumiaji wa dawa za kuua wadudu mara kwa mara kwenye kuta na dari za manyumba hupunguza idadi ya mbu na uwezo wao wa kusambaza ugonjwa huo.
  • Kuondoa maji yaliyosimama na maeneo mengine ya kuzaliana kwa mbu ndani na karibu na maeneo ya makazi kunaweza kusaidia kupunguza idadi ya mbu.
  • Matumizi ya dawa za kufukuza wadudu, kuvaa nguo za mikono mirefu, na kuepuka kukaa nje wakati wa jioni na alfajiri kunaweza kupunguza hatari ya kuumwa na mbu.

SWA.png

Ni muhimu kutambua kwamba malaria haiambukizi na haiwezi kuenezwa moja kwa moja kutoka kwa mtu hadi kwa mtu kama ugonjwa wa mafua, malaria huenezwa na mbu. Kuchukua hatua za kuzuia kuumwa na mbu, kama vile kutumia dawa ya kufukuza mbu, kuvaa nguo za kujikinga, na kulala chini ya neti iliyotibiwa kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya kuambukizwa malaria.

 

Makala Zaidi

Ramani ya Huduma

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820), Jumatatu hadi Jumamosi kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni