Julisha.Info ni sehemu ya mradi wa kimataifa wa Signpost, mradi wa mawakala mbali mbali ambao unatumia mitandao ya kijamii na tovuti kutoa habari na kuwezesha mawasiliano ya pande mbili na watu walio katika hali ngumu, wakiwemo wakimbizi, wanaotafuta hifathi, wahamiaji na watu wamekumbwa na ghasia. Tunakutana na watu kwenye mitandao ya kidijitali ambayo tayari wanayatumia na kutoa maelezo ambayo yanalingana na mahitaji yao mahususi.

Julisha.info ilizinduliwa mwaka wa 2021 na ni mpango ambao umejitolea kikamilifu kutoa taarifa kuhusu huduma na usaidizi unaopatikana kwa wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na jumuiya zinazowahifadhi nchini Kenya. Julisha ni neno la kiswahili lenye maana ya 'Kujulisha' au kitendo cha 'kupitisha habari'. Sehemu ya pili ya jina Julisha imetolewa kutoka kwa neno ' information' na hivyo inakuwa Julisha.Info.

Julisha.info inalenga jamii hizo Kakuma, Daadab, Nairobi, na maeneo ya makazi ya mjini yanayoizunguka ili kuwawezesha kujua haki zao na kufanya maamuzi sahihi kuhusu usalama wao, haki zao na wajibu wao, na jinsi ya kupata huduma. Kama programu zingine za Signpost, Julisha.Info ni jukwaa la huduma za habari sikivu. Hii ina maana kwamba habari tunazoshiriki zinatengenezwa ili kukabiliana na mahitaji ya habari ambayo yanaonyeshwa na jamii tunazohudumia.

Julisha.Info haitoi ushauri wa kisheria au kupanga miadi na UNHCR, DRS, wakala au taasisi za umma, lakini tunaweza kukuelekeza kwenye huduma ambazo zinaweza kukusaidia.

Julisha.info inajumuishwa na timu ya wafanyikazi waliohitimu sana wanaofanya kazi kutafuta habari na kuifanya ipatikane kwa jamii katika  lugha za Kiingereza, Kisomali, na Kiswahili kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info, chaneli ya WhatsApp na tovuti ya Julisha.Info.  Habari hii inatolewa kupitia mabango na video za Facebook, vipindi vya moja kwa moja vya Facebook (Facebook Live), makala na soga za ana kwa ana kwenye Facebook Messenger, WhatsApp na ujumbe mfupi wa SMS. Jumbe zinazotolewa na Julisha.Info zinatokana na mahitaji ya taarifa ya watumiaji wetu, uchanganuzi wa taarifa zinazotafutwa zaidi, mitindo inayoibuka, huduma zinazotolewa na mashirika mengine, matukio ya kalenda na mandhari na matukio ya sasa.

Julisha pia ina ramani ya huduma tunazoshiriki ambayo hutoa maelezo ya kina ya mawasiliano kuhusu watoa huduma kama vile hospitali, wanasheria na vituo vya lugha, ambayo huwafanya kuwa rahisi kufikiwa.

Julisha.info hutoa huduma za aina gani?

Kuna washikadau wengi, ikiwa ni pamoja na serikali ya Kenya kupitia Idara ya Huduma kwa Wakimbizi (DRS), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine yanayotoa huduma, usaidizi wa mali, fursa kama vile kazi, ufadhili wa masomo na usaidizi wa kisheria kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi nchini Kenya. Ingawa huduma hizi nyingi zinapatikana bila malipo, ni changamoto kupata taarifa kuhusu wapi na jinsi huduma na usaidizi unavyotolewa.

Julisha.Info inashughulikia changamoto hii kwa kutoa taarifa sikivu, kwa wakati na sahihi kuhusu jinsi ya kupata huduma, fursa, na usaidizi unaopatikana kwa wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na wenyeji wao nchini Kenya ikiwa ni pamoja na ramani za huduma ndani ya kambi. Tunafanya kazi kwa karibu na washikadau hawa ili kupata maelezo kuhusu mashirika yao, huduma wanazotoa, lini, vipi na gharama inapohitajika. Kisha tunatayarisha maelezo haya kwa njia iliyorahisishwa na kuyapakia kwenye tovuti kwa ufikiaji wa mtandaoni na kila mtu, ikiwa ni pamoja na mashirika mengine ambayo hutoa huduma kwa wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na jumuiya inayowakaribisha.

Swahili.png

Jinsi ya kupokea msaada kutoka kwa julisha.Info 

Ili kufaidika na kupokea taarifa kutoka kwa Julisha.Info, unahitaji: 

Kuwa na simu/kompyuta/kibao au kifaa kingine chochote kinachokuruhusu kuingia mtandaoni. 

Kama ikiwa uwezi ingia kwenye mtandao kupitia simu yako. Unaweza kutuma SMS kwa nambari yetu 0110-601820. 

Fuata Julisha.info kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, na Chaneli ya WhatsApp ya Julisha.Info  ili kupokea ujumbe kuhusu fursa na huduma zinazopatikana kwako ukiwa Dadaab, Kakuma ama Nairobi. 

Iwapo una maswali kuhusu huduma na usaidizi katika kambi, unaweza kuzungumza na timu yetu kwa kututumia ujumbe kupitia Facebook Messenger kwa kubofya 👉hapa , au zungumza nasi pale WhatsApp.

  • Ili kupata maelezo ya mahali pa kupata huduma maalum, anwani za watoa huduma na mahitaji. Nenda kwenye Ramani ya Huduma ya Julisha👉 hapa. 
  • Kuwa balozi wa Julisha.Info katika jamii yako kwa kushiriki habari mara kwa mara kwa marafiki, familia na watu wa jamii yako na kuwaonyesha jinsi ya kufikia julisha.info. 
  • #UlizaJulisha na usaidie KUKOMESHA habari za uwongo na uvumi katika jamii yako. Unaweza kuzungumza nasi kwa SMS, Facebook, na WhatsApp, na tutathibitisha kile ambacho ni KWELI na ambacho ni UONGO. 
  • Tumia fursa za mafunzo na kazi ambazo huchapishwa kwenye mitandao ya Julisha.Info mara kwa mara

Julisha Ambassador SWA.png

Ufikiaji wa Julisha

Tangu kuzinduliwa kwake Machi 2021, Julisha.Info imetoa maelezo ambayo yamesaidia wengi kufanya maamuzi sahihi kuhusu masuala mbalimbali.

Reach & Impact SWA.png

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820) ,Jumatatu hadi Ijumaa kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni