CBC_Jnr_Secondary_Graphic_SWA.png

PICHA:Mwalimu wa kike katika mazingira ya darasani. Makala haya yanaelezea elimu ya sekondari-upeo wa chini nchini Kenya. Chanzo/Julisha.

Jambo la Kuzingatia: Mnamo Oktoba 2022, serikali ya Kenya iliteua jopokazi la kukusanya maoni ya umma kuhusu utekelezaji wa Mtaala unaozingatia Umahiri (CBC) na kutoa mapendekezo. Ukusanyaji wa maoni ya umma ulihitimishwa mnamo Novemba 2022. Kwa sasa serikali inapitia matokeo ya jopokazi hilo. Mara tu mchakato huu utakapokamilika, tutasasisha makala haya ili kujumuisha mabadiliko yatakayofanywa kwenye mtaala.

Elimu ya Sekondari ya  upeo wa chini nchini Kenya inakamilika kwa miaka mitatu chini ya mfumo wa mtaala unaozingatia uwezo (CBC). CBC ni mfumo wa elimu nchini ulioanzishwa Desemba 2017. Chini ya mfumo wa CBC, maendeleo ya kila mwanafunzi yanafuatiliwa katika kipindi cha miaka 2-6-3-3, ikigawanywa kwa usawa katika viwango vitatu vikuu vya elimu:

  • Elimu ya miaka ya mapema
  • Elimu ya shule ya kati
  • Elimu ya shule ya upili, elimu ya juu na chuo kikuu

Elimu ya sekondari upeon upeo wa chini hutumika kama daraja kati ya shule ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 12 hadi 14. Shughuli zote za elimu ya sekondari ya upeo wa chini zimejikita katika elimu inayolingana na umri, ustawi wa wanafunzi na usaidizi wa mpito kwa wanafunzi.

Unaweza kubonyeza hapa ili kujifunza zaidi kuhusu masomo ya msingi, mitihani na elimu nchini Kenya. Kuna masomo ya msingi yanayoteuliwa   kwa wanafunzi wanaoingia gredi yaya saba, nane, na tisa.

Wanafunzi wote katika ngazi ya sekondari ya vijana lazima wachukue masomo yafuatayo:

  1. Kiingereza
  2. Kiswahili au Lugha ya Ishara ya Kenya
  3. Hisabati
  4. Sayansi
  5. Elimu ya afya
  6. Elimu ya awali ya kiuufundi
  7. Masomo ya Jamii
  8. Elimu ya Dini: wanafunzi huchagua mojawapo ya yafuatayo: Elimu ya Dini ya Kikristo, Elimu ya Dini ya Kiislamu au Elimu ya Dini ya Kihindu.
  9. Masomo ya Biashara
  10. Kilimo
  11. Stadi za Maisha
  12. Michezo na Elimu ya Kimwili

Wanafunzi wote wanaoanza shule ya upili ya upeo wa chini lazima wasome angalau somo moja na sio zaidi ya masomo mawiliya kuteua. Masomo teuzi ni pamoja na:

  1. Sanaa za visual
  2. Sanaa za maonyesho
  3. Sayansi ya nyumbani
  4. Sayansi ya kompyuta
  5. Lugha za kigeni (Kijerumani, Kifaransa, Mandarin/Kichina, au Kiarabu)
  6. Lugha ya ishara ya Kenya
  7. Lugha za asili

Ikumbukwe kwamba katika kambi za wakimbizi za Dadaab, shule zitatoa masomo teuzi kulingana na walimu wa masomo wanaopatikana na uwezo wa shule. Shule nyingi za ngazi ya upili zitatoa sayansi ya kompyuta, Lugha ya ishara ya Kenya, Kiarabu na sanaa za maonyesho. UNHCR, kwa kushirikiana na mashirika washirika huko Kakuma na Dadaab inatoa ufikiaji wa bure wa elimu (nyenzo zote za kujifunzia na kufundishia) kwa wanafunzi wote.

Ikiwa wewe ni mkimbizi au mtafuta hifadhi nchini Kenya, unaweza pia kuwaandikisha watoto wako katika shule katika kambi ikiwa una kadi ya mgao au, uthibitisho wa kujiandikisha (Manifest). 

Watoto wanaweza kujiunga na shule kwenye kambi au sehemu zingine za nchi ikiwa unaishi nje ya kambi. Ikiwa huna hati zozote kati ya hizi, mtoto wako bado atakuwa na haki ya kuwa shuleni. Mkuu wa shule lazima afahamishwe kuhusu kupoteaau ukosefu wa nyaraka zinazohitajika.

Maeneo jumuishi ya masomo ya sayansi ya jumla kwa shule za upili-upeo wa chini nchini Kenya

Sayansi ya jumla ni mojawapo ya masomo ya msingi kwa wanafunzi wa darasa la saba, nane na tisa. Ili kufundisha sayansi jumuishi katika ngazi hii, Wizara ya Elimu iliwapa kazi na kuwapa walimu mseto wa masomayaBiolojia/Kemia. Maeneo ya kujifunza yanahusu fizikia, kemia, biolojia, na maelezo ya jumla ya sayansi.

Maeneo ya kujifunzia elimu ya afya kwa shule za sekondari za chini nchini Kenya

Elimu ya Afya ni moja ya masomo ya msingi katika shule ya upili, upeo wa chini. Walimu waliopata mafunzo ya Biolojia/Sayansi ya nyumbani ndio wanaohusika na kutoa malengo ya elimu ya afya. Wanafunzi hufundishwa sayansi ya mazingira, afya ya umma, usafi wa kibinafsi, na lishe katika elimu ya afya.

Elimu ya awali na ya awali ya kiufundi kwa wanafunzi wa shule za upili, upeo wa chini nchini Kenya

Somo hili la lazima linalenga kuwapa wanafunzi ujuzi mbalimbali katika kujitayarisha kwa ajili ya mafunzo ya kiufundi yaliyoimarishwa katika ngazi ya shule ya upili upeo wa juu na elimu ya juu. Walimu wamepewa mafunzo maalum ya kufundisha hisabati, fizikia na sayansi ya nyumbani. Wanafunzi hujifunza kazi za mbao, ufundi chuma, kuchora kiufundi, umeme, usimamizi wa nyumba, uandishi wa chapa,shorthand, auto-mechanics na misingi ya uhasibu.

Mwanafunzi anajiunga vipi na shule ya sekondari?

Kuanzia Januari 2023, mabadiliko ya kwanza kutoka shule ya msingi hadi ya sekondari ya upeo wa chini yatafanyika. Wizara ya Elimu inaruhusu wanafunzi wa darasa la sita kuchagua shule za upili wanazopendelea. Orodha ya shule inatolewa na mwalimu mkuu wa shule anakosoma mwanafunzi. Mnamo Agosti 2022, shule za sekondari upeo wa chini, gredi ya saba mnamo 2023 zilichaguliwa.

Wanafunzi wanaweza kujiunga na shule za umma au za kibinafsi zilizoidhinishwa kutoa elimu ya sekondari ya chini nchini Kenya. Ingawa udahili na masomo katika shule za sekondari za chini za serikali hulipiwa na serikali, wazazi ambao wanaweza kumudu kuwapeleka watoto wao katika shule za sekondari za kibinafsi zilizoidhinishwa wanaweza kufanya hivyo. 

Walimu wakuu wanaweza kufikia orodha ya shule zilizoidhinishwaBaada ya kufaulu mitihani yao ya mwisho wa elimu ya msingi katika gredi ya sita, wanafunzi wanaweza kujiunga na shule za sekondari za chini wanazopenda. Mtihani huu unajulikana kama Kenya Primary School Education Assessment. Mtihani wa KPSEA utafanyika kuanzia Novemba 28 hadi Novemba 30, 2022.

 

Je, mtu huchaguaje shule ya sekondari ya upeo wa chini kwa mtoto wake?

Walezi na wazazi wote wanatarajiwa kushirikiana na walimu wakuu wa shule ili kuwasaidia wanafunzi katika kuchagua shule zinazofaa kwa elimu yao ya sekondari. Walimu wakuu wote walihitajika kuwaongoza wanafunzi wakati wa zoezi la kwanza la uteuzi, lililokamilika Agosti 30, 2022. Baraza la kitaifa la mitihani la Kenya (KNEC)liliwapa walimu wakuu kitengo kwenye tovuti yenye orodha ya shule zote za upili zilizoidhinishwa. Wanafunzi wangechagua kutoka kwa shule zilizopo.

 

Je! ni chaguzi gani za shule za sekondari zinazopatikana kwa wanafunzi?

Wizara ya Elimu inahitaji kwamba kila mwanafunzi achague shule zifuatazo wakati wa kuchagua shule za chini:

  • Shule mbili za kitaifa
  • Shule mbili za Mkoa
  • Shule mbili za kaunti
  • Shule nne za chini za ngazi ya kaunti ndogo
  • Shule mbili za sekondari za kibinafsi

Tafadhali kumbuka kuwa gharama za elimu kwa wanafunzi wanaokubaliwa katika shule za sekondari za kibinafsi zitatozwa na wazazi ambao wamekubali uandikishaji wao. Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, wanafunzi wanatarajiwa kuendelea na shule ya upili. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu elimu ya shule ya upili hapa.

Baraza la kitaifa la mitihani (Kenya National Examination Council) linaweza kupatikana kupitia mawasiliano yanayopatikanahapa.

 

Ikiwaunamaswaliyoyote, tafadhalituandikiekupitiaukurasawa Facebook waJulisha.Info au zungumza nasi kupitiaWhatsApp(+254110601820) ,JumatatuhadiJumamosikutoka 08:00 asubuhihadi 5:00 jioni