Je,wewe ni mfanyi biashara katika kambi ya Dadaab? Je, una wazo ambalo ungependa kuligeuza kuwa biashara? Sasa unaweza kupata usaidizi katika kituo maalum Dadaab, maarufu kama One-stop shop.

Shirika la Danish Refugee Council (DRC), Serikali ya kaunti ya Garissa na idara ya huduma ya wakimbizi (Department of Refugee Services) na watoa huduma wengine katika kambi ya Dadaab wanashirikiana kuleta huduma za usaidizi wa kukuza biashara. Huduma mbalimbali zinazoweza kuimarisha biashara sasa zinapatikana mahali pamoja kwenye kituo hicho maalum kambini Dadaab.

Tunamaanisha nini tukisema huduma zote zinapatikana mahali pamoja?

Kama jina linavyopendekeza, utaenda mahali pamoja, mara moja na kutimiza mahitaji yako. Wenye nia ya kuanzisha au kuimarisha biashara za kibinafsi au katika makundi wanaweza kupata usaidizi chin ya kituo cha huduma katika sehemu moja badala ya mahali tofauti.

Huduma_DOSS.png

Nani anaweza kunufaika na One-Stop-Shop

Huduma zinazotolewa katika vituo hivi zinaweza kufikiwa kila mwezi na wakimbizi, wanaotafuta hifadhi na wanajamii  wanaowapokea. Walengwa wanaweza kujumuisha:

  • Wamiliki wa biashara katika kambi ya Dadaab
  • Vikundi vya kujisaidia, maarufu kama Self-help-groups
  • Mashirika ya kijamii (Community Based Organizations)
  • Mashirika yanayoongozwa na Wakimbizi (Refugee Led Organizations)
  • Watu binafsi wanaotaka kuanzisha biashara

Huduma zinazopatikana One-Stop-Shop

Mashirika mbalimbali, Kaunti ya Garissa, DRS na DRC wanashirikiana kutoa huduma mbalimbali za usaidizi wa biashara na usaidizi katika vituo hivi katika ofisi za DRS huko Dagahaley, Hagadera na Ifo. Unaweza kupata huduma zifuatazo hapa:

  • Usajili wa biashara Unaweza kusoma jinsi ya kusajili biashara hapa
  • Vibali vya biashara na leseni
  • Ukaguzi wa usafi na udhibitisho
  • Huduma za kifedha kama vile mikopo na taarifa
  • Taarifa ya kodi: unaweza kusoma jinsi ya kupata nambari ya kibinafsi ya KRA hapa

Mahali ambapo utapata huduma na usaidizi wa bishara Dadaab

Maeneo ya kutoa huduma hizi hutengwa kila mwezi  katika ofisi za Idara ya Huduma kwa Wakimbizi (Department of Refugee Services) huko Ifo, Dagahaley na Hagadera.

Kila moja ya kambi hizo tatu imepewa siku moja kila mwezi. Ifuatayo ni ratiba ya Julai hadi Desemba 2022. Itazame ili kujua ni lini huduma zitapatikana katika ofisi ya DRS iliyoko karibu nawe.

Kalenda.png

Je, ni nyaraka gani ninapaswa kuleta kwa duka la huduma?

Nyaraka zitategemea aina ya huduma utakayotafuta. Beba angalau:

  1. Kitambulisho/Onyesho la Mkimbizi (uthibitisho wa usajili kwa wakimbizi)
  2. Kitambulisho cha faifa - cha Wakenya

Ni mashirika gani zinatoa huduma kwenye duka la huduma?

Utapata madawati kwa watoa huduma mbalimbali. Hawa ndio watoa huduma walio na madawati yanayofanya kazi kufikia Julai 2022:

  1. Department for Refugee Services (DRS)
  • Taarifa kuhusu wakimbizi na kanuni nyingine za serikali kuhusu biashara
  • Maombi ya kupitisha harakati za biashara
  1. Serikali ya Kaunti ya Garissa
  • Dawati la huduma za jamii hutoa usajili na uthibitisho kwa vikundi vya kujisaidia na mashirika ya kijamii (Community Based Organizations)
  • Dawati la afya ya umma linatoa usaidizi kwa biashara zinazohitaji ukaguzi wa afya ya umma
  • Dawati la biashara kwa ajili ya utoaji wa vibali vya biashara na leseni kwa wafanyabiashara
  1. African Entrepreneur Collective (AEC Kenya)
  • AEC-Kenya inatoa mafunzo na usaidizi wa kifedha na mafunzo kuhusu uwekaji hesabu, misaada, na mikopo kwa biashara zilizoanzishwa Dadaab.
  1. Kenya Chamber of Commerce, Garissa chapter
  • Mafunzo ya biashara na ruzuku zinazolipwa hutolewa kwa biashara zinazostahiki.
  1. Norwegian Refugee Council (NRC)
  • Msaada wa kupata, kubadilisha hati zilizopotea au zilizoharibika,
  • Usaidizi wa masahihisho ya hati za kiraia na utambulisho kama vile vyeti vya kuzaliwa na kifo.

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info au zungumza nasi kupitia WhatsApp (+254110601820), Jumatatu hadi Jumamosi kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni