Je,unajua pa kufikia iwapo unahitaji huduma za afya, kisheria,chakula,elimu,ajira au usaidizi wa huduma za kijamii?

Julisha.Info imeweka pamoja watoa huduma hawa wote na wengi zaidi katika sehemu moja, ambayo tunaita Ramani ya Huduma. Inajumuisha maelezo yote ya huduma; kutoka kwa maelezo ya mawasiliano hadi maeneo ya huduma kuu ambazo zinalenga wakimbizi na wanaotafuta hifadhi.

Taarifa hizo zinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kiswahili, Kisomali na Kiarabu

Ramani ya Huduma ni nini?

Ramani ya Huduma ni saraka inayoweza kutafutwa yenye taarifa kuhusu huduma zinazopatikana kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi katika maeneo fulani nchini Kenya. Maelezo ya huduma yanapatikana kupitia vifaa vilivyounganishwa kwenye mtandao. Ramani ya Huduma hukusaidia kupata huduma kutoka kwa serikali, taasisi za kibinafsi, mashirika ya kimataifa au ya kitaifa yasiyo ya kiserikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, na jumuiya au mashirika ya kidini.

Taarifa ya huduma hii inaangazia maeneo ambayo yana idadi kubwa ya wakimbizi na wanaotafuta hifadhi, hasa Eneo la Jiji la Nairobi, na Kaunti za Turkana na Garissa.

Nani anaweza kufikia Ramani za Huduma?

Ramani ya Huduma inapatikana kwa wote walio na muunganisho wa internet. Tafadhali bonyeza hapa ili kufikia Ramani ya Huduma. Ingawa mtu yeyote anaweza kufikia Ramani ya Huduma, maelezo ya huduma yanalenga sana huduma zinazotolewa kwa wakimbizi na wanaotafuta hifadhi nchini Kenya.

Tunaweka kila juhudi kutoa taarifa sahihi za huduma. Kabla hatujachapisha habari, taasisi inayotoa huduma huangalia na kukubaliana nayo. Pia tunasasisha habari mara kwa mara.

Je, Ramani ya Huduma ina nini ya kutarajia?

Ramani ya Huduma inajumuisha maelezo yote ya huduma, ambayo husaidia kuwawezesha wakimbizi na wanaotafuta hifadhi kukidhi mahitaji yao kwa ufanisi zaidi kwa kuwaunganisha na huduma wanazohitaji. Maelezo hayo yanajumuisha taarifa za mawasiliano za taasisi, saa za kazi, anwani na viwianishi vya maeneo, upatikanaji wa huduma kwa watu mbalimbali wenye mahitaji tofauti, na vigezo vya kustahiki vinavyohitajika ili kupata huduma.

Taarifa hizo pia zinajumuisha mbinu za watoa huduma za kutoa maoni ambazo kwazo wakimbizi na wanaotafuta hifadhi wanaweza kuibua masuala na wasiwasi kwa taasisi.

Picture23.png

Picha inayoonyesha mfano wa huduma katika ramani ya huduma ya kurasa ya Julisha.Info 

Mwongozo wa hatua wa jinsi ya kutumia Ramani ya Huduma ya Julisha.Info

Kuna chaguo mbili za kupata Julisha.Info Service Information

Chaguo 1: Bonyeza kwenye Ramani ya Huduma kwenye sehemu ya juu kulia ya tovuti ya Julisha.Info.

Picture111.png

Ukurasa ulio hapa chini utaonekana ukikupa chaguo tatu (3) kutoka mahali pa kutafuta maelezo ya huduma:

  1. Unaweza kuchuja huduma kutoka kategoria za huduma kwenye chaguo kunjuzi.
  2. Bonyeza mahali unapohitaji huduma kwenye ramani, na utaongozwa na aikoni za aina za huduma ili kutambua huduma unazohitaji katika maeneo yaliyopangwa.
  3. Bonyeza kwenye eneo lililolengwa upande wa kulia, na utaongozwa kwa miji ndani ya mikoa na huduma zilizomo.

Picture333.png

Chaguo la 2: Unaweza pia kufikia huduma kwa kubofya "Huduma" kwenye tovuti ya Julisha.Info.

Mfano:

Ufuatao ni mfano wa ukurasa utakaoongozwa ikiwa unahitaji maelezo ya huduma kutoka eneo la Nairobi Metropolitan.

Picture444.png

Ili kupata taarifa za huduma zinazohitajika, kwa mfano kutoka eneo la Nairobi Metropolitan, fuata mojawapo ya chaguo tatu hapa chini:

  1. Chuja huduma kutoka kwa orodha za huduma kwenye chaguo kunjuzi, a
  2. Bonyeza kwenye ramani, eneo linaloonyesha idadi ya huduma katika eneo hilo, na utaongozwa na aikoni za kategoria ya huduma ili kutambua huduma unazohitaji katika maeneo yaliyopangwa, au
  3. Bonyeza kwenye mji unaolengwa kwenye upande wa kulia, na utaongozwa kwenye ramani na makala yenye maelezo ya huduma.

Ifuatayo ni mfano wa mahali utakapoelekezwa ukibonyeza Jiji la Nairobi.

Picture55.png

Ili kupata taarifa za huduma zinazohitajika, kwa mfano kutoka Jiji la Nairobi, fuata mojawapo ya chaguo tatu hapa chini:

  1. Chuja huduma kutoka kwa kategoria za huduma kwenye chaguo kunjuzi, au
  2. Bonyeza kwenye ramani, eneo linaloonyesha idadi ya huduma katika jiji, na utaongozwa na aikoni za kategoria ya huduma ili kutambua huduma unazohitaji katika maeneo yaliyopangwa, au
  3. Bonyeza kwenye huduma upande wa kulia, na utaongozwa kwa makala na maelezo ya huduma.

Ukiwa unataka shirikisho lako lijumuishwe kwenye kurasa ya ramani ya Julisha.Info Service Map, tuma barua pepe kwa Jodom.Nyambati@rescue.org au Victor.Achok@rescue.org 

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu huduma za uzazi kwa wakimbizi nchini Kenya, tafadhali tuandikie kupitia ukurasa wa Facebook wa Julisha.Info, Jumatatu hadi Ijumaa kutoka saa 2 hadi saa 11 jioni.