Chanjo ya Covid-19 ilianza kutolewa mnamo Machi 2021 nchini Kenya, na mwanzoni mwa zoezi la chanjo, kundi lililolengwa lilikuwa wafanyikazi wa mstari wa mbele ikiwemo wafanyakazi wa afya, watoa huduma muhimu kama vile walimu na wafanyakazi wa usalama, na watu wenye umri wa zaidi ya miaka 58. Kwa sasa, chanjo ya Pfizer inatolewa kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15-17. 

Kwa nini nipate cheti cha chanjo ya Covid-19?

Cheti cha chanjo ya COVID-19 ni dhibitisho kwamba umechanjwa dhidi ya virusi vya COVID-19. Kuongezeka kwa upatikanaji wa chanjo duniani kote kwa wakati mmoja kumesababisha kuongezwa kwa mahitaji ya chanjo na serikali mbalimbali ili mtu aweze kuingia katika nchi zao. Ingawa chanjo si ya lazima, kutokuwepo kwake kunaweza kusababisha watu ambao hawajachanjwa kukabiliwa na  vikwazo kama vile kupima mara kwa mara, au kutengwa. Mtu yeyote ambaye amechanjwa nchini Kenya anaweza kupata cheti chake cha chanjo ya Covid-19 mtandaoni. 

Tovuti ya Chanjo Kenya

Wizara ya Afya nchini Kenya ilizindua tovuti ya huduma binafsi, inayojulikana pia kama Chanjo Kenya, ili kuwasaidia wakazi wote nchini Kenya kuifuata michakato ya Chanjo ya Covid-19 kama vile:

  • Kujiandikisha kwa chanjo
  • Kutazama ratiba ya chanjo
  • Kutazama maelezo yako ya usajili kwa chanjo ya Covid-19
  • Kusasisha maelezo ya usajili wa chanjo ya Covid-19
  • Kupakua cheti cha chanjo ya Covid-19
  • Kuthibitisha cheti chako cha chanjo ya Covid-19 nchini Kenya

Katika makala haya, tutaelezea mchakato wa kupata cheti chako cha chanjo ya Covid-19 kutoka Tovuti ya Chanjo Kenya.

Nani anaweza kupata cheti cha chanjo ya Covid-19?

Mtu yeyote ambaye amepokea dozi ya kwanza ya chanjo za Astra Zeneca, Moderna au Pfizer anaweza kujisajili, kuangalia tarehe ya kupata dozi yake ya pili, na kupakua cheti chake cha chanjo ya COVID-19 kupitia tovuti hii. Chanjo ya Johnson na Johnson inatolewa kwa dozi moja na hivyo unaweza kupata cheti chako cha chanjo hiyo mara tu unapopata chanjo.

Jinsi ya kupata cheti chako cha chanjo dhidhi ya Covid-19:

COVID_VACCINE_CERTIFICATE_DOWNLOAD_INFOGRAPHIC_SWA.png

Mwongozo unaoonyesha hatua za kupakua Cheti chako cha chanjo ya Covid-19

Hatua ya Kwanza: Tembelea Tovuti ya Chanjo Kenya 

Tembelea tovuti ya Wizara ya Afya ya kujihudumia hapa na ubofye kitufe cha "Pata Huduma" chini ya Tovuti ya Chanjo (MOH NVIP)

Chanjo_Kenya_Portal_SWA.png

Picha inayoonyesha mahali pa kubofya ili kufikia tovuti ya Chanjo ya Covid-19 kwenye tovuti ya huduma binafsi ya Wizara ya Afya.

Utaelekezwa kwenye tovuti ya chanjo Kenya ambapo utaombwa kuunda akaunti. Ikiwa tayari una akaunti, ingia kwenye akaunti hiyo.

Chanjo_Kenya_Home_page.png

Picha ya ya ukurasa wa kwanza wa tovuti ya Chanjo Kenya.

Hatua ya Pili: Fungua akaunti  

Bofya kwenye "Fungua Akaunti/Create Account", utahitajika kutoa maelezo fulani, ikiwa ni pamoja na aina ya kitambulisho chako, pamoja na nambari ya Hati ya Utambulisho (Kitambulisho). Aina ya kitambulisho inaweza kuwa:

  • Kitambulisho cha Taifa
  • Pasipoti
  • Cheti cha Kuzaliwa
  • Kitambulisho cha Mgeni
  • Kitambulisho cha Kijeshi

Mara tu unapoingia kwenye tovuti ya Chanjo Kenya na kubonyeza "Unda Akaunti" utaulizwa ikiwa umechanjwa au la.   

Vaccinated_Yes_No.png

Unapofungua akaunti yako, tovuti inakuhitaji uchague ikiwa umechanjwa au la

Hatua ya Tatu: 

A. Ikiwa umepata chanjo: 

Ikiwa umepata chanjo, utahitajika kuingiza Aina ya Kitambulisho na Nambari ya Kitambulisho ulichotumia wakati wa kujiandikisha, au ile uliyotoa kwenye kituo cha chanjo.

*Tafadhali chagua Aina ya Kitambulisho ulichotumia wakati wa kupata chanjo kwenye kituo cha afya.

Hakikisha kuwa umeweka maelezo yako kwa usahihi na ubonyeze “Tafuta/Search”. Utaona maelezo uliyotoa kwenye kituo cha chanjo.

Vaccinated_Yes.png

Picha inayoonyesha maelezo yanayohitajika ili kuunda akaunti ikiwa umechanjwa

B. Ikiwa hujapata chanjo:  

Iwapo hujapata chanjo, utaombwa kuchagua aina ya kitambulisho ambacho utatoa kwenye kituo cha afya wakati wa chanjo.

Vaccinated_No.png

Picha ya skrini ya maelezo yanayohitajika ili kuunda akaunti ikiwa hujachanjwa.

Hakikisha kuwa maelezo unayotoa unapofungua akaunti yako ni sahihi. Jina la kwanza, jina la kati na jina la mwisho ni maelezo ambayo yataonekana kwenye cheti chako cha chanjo ya Covid-19.

Pia utahitajika kutoa maelezo kama vile jinsia yako, tarehe ya kuzaliwa, maelezo yako ya mawasiliano, na nchi yako ya asili.

Hatua ya nne: Pakua Cheti chako

Ikiwa umechanjwa kikamilifu - kumaanisha kuwa umepata dozi mbili za chanjo ya Astra Zeneca, Moderna au Pfizer, au dozi moja ya chanjo ya Johnson & Johnson- unapaswa kuona kitufe cha 'Cheti cha Chanjo'.

Unapobofya kitufe hiki, utaona Cheti chako cha Chanjo ya Covid-19 na chaguo la kuipakua kama faili ya PDF.

Cheti cha Chanjo ya COVID-19 nchini Kenya inapaswa kuonekana kama hii:

Vaccine_Cert-Eng.png

Picha ya skrini ya Cheti cha Chanjo ya Covid-19.

Nitafanya nini ikiwa ninatatizika kupakua cheti changu cha Chanjo ya Covid-19 kutoka kwa tovuti ya Chanjo-Kenya?

  1. Ikiwa ulipata chanjo yako huko Kakuma au Dadaab, unaweza kutembelea kituo cha afya ambapo ulichanjwa, na utasaidiwa kupata cheti chako cha chanjo. Hakikisha kuwa una hati zako za utambulisho.
  2. Unaweza kupitia sehemu ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs) kwenye ukurasa wa nyumbani wa tovuti ya Chanjo Kenya na utapata majibu kwa baadhi ya masuala ya kawaida yaliyozuka.
  3. Tembelea ukurasa wa usaidizi wa Chanjo Kenya na uwasilishe suala lako.

Kwenye ukurasa wa usaidizi, utahitajika kutoa:

  • Anwani yako ya Barua pepe
  • Nambari ya simu uliyotumia kujiandikisha kwa chanjo
  • Aina ya kitambulisho ulichitumia kujiandikisha wakati wa chanjo
  • Maelezo kuhuzu suala lako kwa undani

Chanjo_Kenya_Help_Page.png

Picha ya  ukurasa wa usaidizi wa Chanjo Kenya ambapo unaweza kuripoti matatizo yoyote yanayotokea kwenye tovuti.

 

Tazama VIDEO HII ya wizara ya afya ili kuelewa jinsi ya kutumia tovuti ya Chanjo Kenya.

Pata hapa habari zaidi kuhusu Chanjo ya Covid-19 nchini Kenya.

Ikiwa una maswali yoyote, unaweza kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa Facebook ama WhatsApp (+254110601820) Jumatatu hadi Ijumaa kutoka 08:00 asubuhi hadi 5:00 jioni.