Duniani kote soka ni mchezo ambao uko na umaarufu mkubwa. Nchini Kenya inafuatwa kwa karibu na riadha na mchezo wa raga kama michezo inayoshabikiwa zaidi.Umaarufu wa soka unaanzia watoto wachanga hadi walio wakongwe kwenye jamii.

Kutokana na mkurupuko wa ugonjwa wa COVID-19 ni muhimu kwa wachezaji na makocha kuzingatia kanuni za serikali kukabiliana na ugonjwa huu kambini na hata nje ya kambi.

Kupunguza kusambaa kwa ugonjwa huo wanaspoti wanahimizwa kuchanjwa dhidi ya ugonjwa huo.

Jinsi ya kuzuia kusambaa kwa COVID-19?

  • Kunawa mikono kila wakati kwa kutumia sabuni na maji kabla na baada ya mechi.
  • Kutumia kidudufishaji au sanitizer
  • Kukohoa au kupiga chafya kuelekea kiwiko cha mkono wako au kitamba
  • Hakikisha vifaa vya mchezo kama mipira, neti na sare zimeoshwa kabla ya matumizi
  • Usikubali kutumia taulo na mtu mwengine.
  • Epuka kuguza uso, macho na mdomo.

 

Wachezaji wanaweza kuvaa barakoa wakati wa mechi?

Muungano wa afya duniani WHO hairuhusu kutumika kwa barakoa wakati wa mazoezi au hata mechi. Hii ni kwa sababu barakoa yaweza kuloa na kusababisha ugumu wakati wa kupumua.

Hata hivyo wale ambao hawatakuwa uwanjani wanahimizwa kuvaa barakoa na kutokaribiana.

Nini cha kufanya Ikiwa mchezaji amepatikana na COVID-19.

  • Ikiwa mchezaji amepatikana kuwa na virusi au ametengamana na na mtu aliyena virusi hivyo basi asihudhurie mazoezi au kushiriki mechi yoyote.
  • Makocha na wasimamizi wanapaswa kuwajilisha wahudumu wa afya katika kuhusu dalili zozote za ugonjwa huo.
  • Makocha wanapaswa kuwa na orodha ya wachezaji wote na nambari zao za simu.

Je timu nzima inahitajika kuenda karantini ikiwa mmoja wao amepatikana na virusi?

Ili kujikinga na kukinga wenzako unapaswa kusalia nyumbani kwa siku tano na kuzingatia maagizo ya Wizara ya Afya nchini.

Wachezaji kupitia wasimamizi wanapaswa kuhusisha wahudumu wa afya kubaini hali ya timu hiyo.

Ikiwa kuna fursa ya kupima. Wachezaji wanahimizwa kupimwa baada kutoka karantini.

 

Je wasimamizi wako na jukumu gani katika kupambana na COVID-19?

  • Kuelimisha makocha na wachezaji jinsi ya kutabiri dalili za mapema.
  • Kuelimisha wachezaji na makocha kuhusu mbinu za kujikinga wakati wa mechi na mazoezi.
  • Kuhakikisha kuwepo kwa sabuni, maji na vidudufishaji au sanitizer uwanjani.
  • Kuhakikisha masharti ya wizara ya afya yamezingatiwa.
  • Kuweka mabango au matangazo mahala ambapo wachezaji wataweza kuona kwa virahisi, kuhusu athari za COVID-19.

 

Iwapo una maswali yoyote kuhusu unyonyeshaji,wasiliana nasi kupitia ukurasa wa Julisha.Ifo kwenye mtandao wa Facebook,kila Jumatatu hadi Ijumaa kutoka saa 08:00 asubuhi hadi  5:00 jioni.