mceclip0.png

Mtoto mchanga anayenyonya. Kila mwaka, siku saba za kwanza za mwezi wa Agosti hutumiwa kusherehekea siku ya kunyonyesha duniani. [Picha:Kwa Hisani]

Watoto wana mahitaji yao na njia zao binafsi za kujieleza.  Kulia ni lugha watoto wachanga hutumia kuwasiliana hapa ulimwenguni ,haswa na mama zao.

Wakati mwingine, inaweza fadhaisha mama anayepata taabu kuelewa lugha hii, haswa mtoto anapokataa kunyonya.

Katika hali hii, familia yako na wasaidizi huwa na hofu na kushangaa tatizo linalomkera mtoto. Ni ngumu kumtuliza mtoto mchanga ambaye hawezi kunena.

Watoto hulia zaidi wakati:

  • Adha wanazokabiliana nazo ni unyevu au joto, uchovu,magonjwa/maumivu au wakati wanahitaji uangalifu.
  • Wakati mtoto anataka kunyonyeshwa: Wakati mwingine haswa wiki ya pili, wiki ya sita na miezi tatu, mtoto huwa anakua kwa haraka. Hii huwafanya wahisi njaa. Kunyonyesha mara mingi hukupa hakikisho kuwa mtoto anapata maziwa ya kutosha ili aweze kukuwa ipasavyo.
  • Msokoto (Colic): Colic ni wakati mtoto mwenye afya analia mara kwa mara bila sababu wazi. Inafafunuliwa kama kulia kwa zaidi ya masaa matatu kwa siku angalau siku tatu kwa wiki kwa zaidi ya wiki tatu. Colic sio ugonjwa lakini mchanganyiko wa tabia zisizoeleweka na hakuna suluhisho ila tu kupita kwa wakati.

Suluhisho zinazopendekezwa:

  • Shika mtoto kwa tumbo
  • Shikilia mtoto kwa kifua cha mamaili kupunguza maumivu.
  • Shikilia mtoto kwa kigasha
  • USIMPE mtoto maji ya gripe na maandalizi mengine kwa kuwa hayatasaidia.
  • Hakikisha mtoto ananyonya titi ipasavyo.
  • Saidia mtoto kupitisha hewa kila anapomaliza kunyonya.
  • USIMPE mtoto chochote hadi daktari wako akupe mawaidha zaidi.
  • Colic huwa inaisha. Watoto wengi huzidi wakati wana umri wa miezi tatu na nne na kwa sababu mtoto wako ana colic haimanishi kuwa hawana afya.

Kunyonyesha kunachangia kuishi, afya na ustawi wa sio mtoto tu, bali sisi sote.Kwa hivyo ni jukumu la pamoja.

Kila mwaka,siku saba za kwanza katika mwezi wa Agosti zimetengwa na kuwekwa alama ulimwenguni kama wiki ya kunyonyesha duniani. Julisha.Info inachukua hafla hii maalum kushiriki nanyi vidokezo juu ya kushughulikia kulia kwa watoto na msaada wa familia yako katika kuhakikisha unyonyeshaji sahihi.

Kila mtu katika familia, sio tu mama, anaeza kuhakikisha kuwa watoto wananyonyeshwa vizuri kwa:

  • Kumpa mama mahali pazuri pa kukaa na kumsaidia katika kutunza na kudhibiti watoto wakubwa wakati ananyonyesha mtoto mchanga.
  • Hakikisha mtoto wako ananyonyesha ya kutosha.
  • Kutoa msaada kwa kina mama wanaonyonyesha kwa kusaidia kwa kazi za nyumbani.
  • Assisting the mother in feeding the baby with expressed breast milk when the mother is away for work or any other engagements.
  • Kusaidia mama kumlisha mtoto wakati mama yuko kazini au kwenye shughuli za nyumbani.
  • Kusaidia mama kula vyakula vya afya ili kupata virutubisho vyote mwili inayohiytaji na kwa mtoto pia.

mceclip6.png

Faida za unyonyeshaji wa kipekee

Unyonyeshaji wa kipekee inamaanisha kuwa mtoto mchanga hupokea maziwa ya mama kipekee.Hakuna vimiminika na vitu nyingine yoyote inafaa kupewa mtoto.Watoto wachanga wanapaswa kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza ya maisha ili kufikia afya bora.

Baada ya hapo,ili kukidhi mahitaji ya mtoto ya lishe,watoto wachanga wanapaswa kupata chakula cha kutosha na salama wakati wanaendelea kunyonyesha hadi miaki miwili au zaidi.

  • Kunyonyesha inampa mtoto virutubisho vyote anavyohitaji kwa miezi sita za kwanza ya maisha.
  • Maziwa ya mama yana maji ya kutosha kukidhi kiu ya mtoto hata wakati wa joto.
  • Maziwa yana faida za lishe ambazo huwakinga watoto kutoka magonjwa ya kawaida.
  • Maziwa ya mama ni halisi na tayari kwa mtoto.

Ni muhimu kutambua kuna sababu mingi mama huacha kunyonyesha na kuanza kuchanganya chakula kwa watoto zinaweza kushinda. Kuna mambo kadhaa na muhimu ya kushiriki:

Je, ni kweli kwamba akina mama wengine hawana maziwa ya kutosha? 

LA! Kila mama ako na uwezo wa kutoa maziwa ya kutosha kwa mtoto. Ni nadra sana mama kuweza kunyonyesha mtoto kwa kipekee.

  • Iwapo mama atapata ugumu wa kunyonyesha anashauriwa kuwasiliana na daktari kwa maelezo zaidi.
  • Mtoto wako anapata maziwa ya kutosha anapoongeza kilo nusu kila mwezi katika miezi sita ya kwanza.
  • Mtoto anapovuruta chuchu ya titi ipasavyo,maziwa hutoka kwa wingi.

Je, mama anafaa kuacha wakati mtoto anakataa kunyonyesha?

Hapana, haupaswi kwa kuwa kuna sababu ambazo zinaweza kusababisha hio na inaweza kubadilishwa.

Endelea kujaribu, badilisha nafasi za kunyonyesha, epuka usumbufu na badilisha utaratibu wa mtoto.Mtoto anaweza kuonekana kukataa kunyonyesa kwa sababu ya ugonjwa, mabadiliko ya ghafla ambayo humkasirisha au kwa sababu ya hatua za ukuaji kama kuvuruga.

Kuweka mtoto wako karibu na wewe na mawasiliano ya ngozi kwa ngozi itasaidia mtoto wako kunyonyesha tena.

 

Iwapo una maswali yoyote kuhusu unyonyeshaji,wasiliana nasi kupitia ukurasa wa Julisha.Ifo kwenye mtandao wa Facebook,kila Jumatatu hadi Ijumaa kutoka saa 08:00 asubuhi hadi  5:00 jioni.