Chanjo ya COVID-19 inaendelea kutolewa kwa wafanyikazi wa mstari wa mbele-watu wanaofanya kazi katika sekta za afya, elimu, na usalama - na kwa watu wenye umri zaidi ya miaka 58. 

Watu wengi ambao wamepokea chanjo hiyo wameripoti kuhisi uchungu kwenye mkono ambao ulidungwa, homa, baridi, uchovu, na maumivu ya kichwa kwa siku moja au mbili. Walakini, dalili hizi huhesabiwa kuwa ndogo, na zinaonyesha kuwa mwili unajenga kinga. 

SWAHILI_Covid_Vaccine_Side-Effects.png

Hapa tunataangalia uvumi kadhaa zinazosambaa kuhusu chanjo ya COVID-19 na kuyalinganisha na ukweli uliotafitiwa vizuri. 

          1. Wanaume watakuwa wagumba wakichanjwa 

Utafiti bado unaendelea, lakini hadi sasa hakuna ushahidi wowote kwamba chanjo za COVID zinaweza kusababisha utasa. Wakati utafiti zaidi unafanywa kuhusu chanjo ya COVID-19, wataalamu wa afya wanahimiza watu zaidi kupata chanjo kwani athari zake ni nyepesi na zitakulinda usipate magonjwa kali. 

           2. Sihitaji kupata chanjo kwa sababu tayari nilipata ugonjwa wa COVID-19. 

Hakuna utafiti wa kutosha unaoonyesha muda ambao kinga ya virusi itadumu baada yako kupata

COVID-19. 

Maafisa wa huduma ya afya wanapendekeza upate chanjo, hata ikiwa umewahi kuwa na virusi vya

COVID-19 kwa sababu ya hatari kubwa za kiafya zinazosababishwa na virusi na kwa sababu ya uwezekano wa kuambukizwa tena - ikimaanisha unaweza kupata ugonjwa wa COVID-19 zaidi ya mara moja. Chanjo hukupa kinga bora kutoka kwa aina mbaya ya magonjwa. 

           3. Chanjo ina ina kidude ambach hutumiwa kufuatilia watu. 

Uvumi huu hauna msingi wowote. Hakuna ushahidi au sababu inayoonyesha kwamba chanjo za

COVID-19 zina kidude ambacho hutumiwa kufuatilia watu na kuchukua habari zao za kibinafsi. Chanjo za COVID-19 zilitengenezwa ili kuzuia watu kuambukizwa na virusi vya COVID-19. 

         4. Nitapata ugonjwa wa COVID-19 kupitia kwa chanjo.  

Huu ni uongo. Chnajo ya COVID-19 haina virusi hai, kwa hivyo haiwezi kusababisha maambukizo. Chanjo inafanya kazi kwa kuufanya mwili wako utengeneze protini inayotuambukiza na virusi. Kwa kutengeneza protini hii, mwili wako unakuzuia kuambukizwa. Madhara ambayo unaweza kupata baada ya kupata chanjo - homa, maumivu ya mwili- husababishwa na mwili wako kujifunza kutambua protini hiyo ili iweze kuweka majibu ya kinga. Ikiwa utapata COVID-19 baada ya kupata chanjo, dalili hazitakuwa mbaya sana. 

Tazama video hii kuelewa zaidi jinsi chanjo zinavyofanya kazi. 

         5. Sio lazima kuvaa barakoa au kuweka nafasi kati yang una watu wengine baada ya kupata chanjo.  

Chanjo ya COVID-19 inawakinga watu dhidhi ya kupata dalili kali za ugonjwa wa COVID-19. Hakuna uthibitisho kwamba chanjo hii inazuia kuenea kwa virusi kwa hivyo, njia bora ya kuweka kila mtu salama kutoka kwa virusi vya COVID-19 ni kufuata hatua kama vile kuvaa barakoa, kuweka umbali wa angalau mita 1 kati yako na wengine watu, na kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji. Kuna uwezekano kwamba bado unaweza kupata virusi ingawa dalili zake zitakuwa nyepesi, na bado unaweza kuisambaza kwa wengine. 

               6. Chanjo inaweza kusababisha kifo 

Kumekuwa na uvumi mwingi unaosamba ulimwenguni kote kuhusu watu kufa baada ya kupata chanjo ya COVID-19. Walakini, katika visa vingi ambavyo viliripotiwa, maafisa wa afya na mamlaka katika nchi tofauti hawajapata uhusiano wowote kati ya chanjo na vifo.hivyo. 

              7. Chanjo ilitiengenezwa ili kuwaangamiza wakimbizi. 

Chanjo ya COVID-19 ilitengenezwa ili kuzuia watu kuambukizwa na virusi vya COVID-19 na sio kuwangamiza watu kutoka sehemu tofauti za jamii.  Wakenya na wageni, pamoja na wakimbizi, wanaopewa chanjo nchini Kenya wanapokea chanjo ya Astra Zeneca ambayo inasambazwa na Wizara ya Afya (MoH) kwa kaunti zote nchini kote. 

          8. Chanjo ya COVID-19 inapaswa kutolewa kwa wanawake wazee tu kwani wao ndio waliopita umri wa kuzaa. 

Hakuna ushahidi kwamba chanjo inaweza kuathiri uzazi wa wanawake. Walakini, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linapendekeza kwamba wanawake wajawazito wanapaswa kupata chanjo tu baada ya kujadili na daktari wao kwani faida za kupata chanjo hiyo zinazidi hatari zake. Wanawake wanaonyonyesha wanaweza pia kupata chanjo na kuendelea kunyonyesha. 

     9. Vijana hawahitaji chanjo kwa kuwa hawana hatari ya kupata madhara makali ya ugonjwa wa Covd-19. 

Kwa sasa, majaribio ya chanjo kwa watoto yanafanywa katika sehemu tofauti za ulimwengu na WHO itatangaza wakati chanjo zitakuwa salama na tayari kupatiwa watoto. Chanjo za sasa za Covid zimeidhinishwa kwa watu wenye umri wa miaka 18 na zaidi kwa sababu virusi vya COVID-19 vimeonyeshwa kuwa na athari mbaya zaidi kwa watu wazima. 

             Je, chanjo ni salama? 

Ndio, usalama wa chanjo unapewa kipaumbele, na hii sio tofauti kwa chanjo za COVID-19. Chanjo zote hupitia awamu za majaribio ya kikliniki kabla ya kupitishwa kutumiwa. Majaribio haya yanalenga kuhakikisha usalama na uwezo wa chanjo ya kujikinga dhidi ya ugonjwa (ufanisi). 

SWAHILI_Vaccine_Safety.png

Chanjo zilizotengenezwa dhidi ya COVID-19 zinafuata awamu hizi hizi. Chanjo za COVID-19 hazitakubaliwa au kuletwa kutumika hadi usalama wao utakapothibitishwa na wakala wa udhibiti. Vivyo hivyo, WHO haitatoa chanjo hadi Orodha ya Matumizi ya Dharura ichanganue data zote za majaribio. Baada ya chanjo za COVID-19 kupitishwa, ufuatiliaji wa usalama unaendelea.

Ufuatiliaji huu ni sehemu ya kawaida ya mipango ya chanjo na hufanywa kwa chanjo zote. 

 

Iwapo una maswali yoyote, wasiliana nasi kupitia ukurasa wa Julisha.Info kwenye mtandao wa 

Facebook, kila Jumatatu hadi Jumamosi kutoka saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni.